– Junet alichapisha picha moja kuonyesha mkoba uliokuwa umezua mjadala ni wa nani
– Hata hivyo baadhi ya wanamtandao walikosa kuamini picha hiyo na kusema ameifeki tu ndio kumaliza ukweli
– Wengi waliamini mkoba huo ni kipusa mmoja tajika anayedaiwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Gavana 001
Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed Alhamisi, Julai 9 alilazimika kuonyesha mwanadada waliyeandamana naye Dubai kumuona kinara wa ODM Raila Odinga.
Junet alifanya hivyo baada ya wanamtandao kudai yeye na Gavana Hassan Joho walikuwa wameandamana na vipusa ili wajivinjari.