– Waziri Kagwe amesema hamujui wala hajamlipa mhubiri Robert Burale kujifanya anaugua ugonjwa wa corona
– Hii ni baada ya mhubiri huyo kupakia video mitandaoni akiwajuza mashabiki kuhusu hali yake ya kiafya akiwa hospitalini
– Wakenya wengi wametilia shaka iwapo kweli mhubiri huyo anaugua ugonjwa huo
Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema kuwa hamjui mhubiri Robert Burale wala hajamlipa pesa zozote ili ajifanya kuwa anaugua kutokana na maradhi ya ugonjwa wa COVID-19.
Kagwe alikuwa anajibu madai kuwa serikali imemlipa mhubiri huyu ili awadhibithishie Wakenya kuwa ugonjwa huu upo.
Waziri Kagwe akana madai kuwa amemlipa Robert Burale kujifanya mgonjwa wa COVID-19 Source: UGC
Akizungumza akiwa kaunti ya Mombasa Alhamisi, Julai 9, Kagwe alisema anaamini mhubiri huyo ni mgonjwa baada ya kuona video yake akiwa hospitalini ikisambaa mitandaoni.
” Nimesikia kuhusu jamaa anayeitwa Robert Murathe, hata mimi mwenyewe simfahamu, Kagwe alisema ila wanahabari walimsahihisha kuwa anaitwa Burale wala sio Murathe.
” Nashangaa nimesika kwamba Burale amelipwa ili ajifanywe anaugua COVID-19, sielewi ni nini kinachoendelea, kusema ukweli hata simjui huyu jamaa,” Kagwe aliongezea.