– Kagwe aliwavunja mbavu waandishi wa habari wakati alitishia kuwaanika maafisa wakongwe ambao wamekwamilia afisini mwake
– Alisema ni jambo la busara kustaafu pasi na kuvutana wakati umri wako unapotimia
– Haya yanajiri mwezi mmoja baada ya kutokea mvutano katika jumba la Afya wakati maafisa wanne wa Wizara ya Afya walikataa kuhamishwa
– Kagwe alifanya uhamisho huo baada ya ripoti kutokea kuhusu kutoweka kwa mamilioni ya pesa
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe aliwachekesha waandishi wa habari wakati akitoa takwimu za COVID-19 Jumanne, Julai 7 baada ya kutishia kuwaanika maafisa ambao wamekataa kustaafu afisini mwake.
Kagwe alikuwa akijibu swali huwahusu maafisa katika wizara yake ambao umri wao wa kustaafu umetimia lakini wangali wamekwama katika nyadhifa zao.
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alisema ni jambo la busara kustaafu pasi na kuvutana wakati umri wako unapotimia. Picha: Ministry of Health. Source: UGC
“Hatutaki kumuaibisha yeyote. Kama umehudumia Wizara ya Afya, haijalishi kwa muda upi lakini wakati umri wako wa kustaafu umewadia, tafadhali nenda nyumbani kwa usalama na kwa heshima. Nenda ukawapungie wafanyikazi wenzako kwaheri,” alisema.
Waziri huyo aliwavunja mbavu maafisa wa afya waliokuwepo katika kikao hicho na wanahabari wakati alisema atalazimika kuwapigia simu wajukuu wa maafisa hao.