Wagonjwa wengine 733 waliripotiwa kupata nafuu huku vifo 56 zaidi vinavyotokana na virusihatari vya corona vikirekodiwa.
Picha ya miraa. Source: Facebook
Idadi ya wagonjwa 811 wa Covid-19 kutoka Mombasa wamelazwa hospitalini huku wengine 335 wakihudumiwa kutoka nyumbani.
Hata hivyo Naibu Gavana William Kingi alisema licha ya kwamba Mombasa iko katika hatari zaidi ya kuenea kwa virusi hivyo, maambukizi yamekuwa yakipungua kwa siku za hivi karibuni.
“Hii ni kutokana na mikakati ambayo tumeweka na kwamba wakazi wamekuwa wakiyatilia maanani,” Kingi alidokeza.
Kagwe alitoa heko kwa uongozi wajimbo hilo akisema ni mojawapo ya kaunti ambazo zimejitayarisha vilivyo katika kupambana na janga hilo ambalo limetikisa ulimwengu mzima.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.