Connect with us

General News

Kampeni za kiti cha ugavana Meru zaanza kushika kasi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kampeni za kiti cha ugavana Meru zaanza kushika kasi – Taifa Leo

Kampeni za kiti cha ugavana Meru zaanza kushika kasi

Na DAVID MUCHUI

KINYANG’ANYIRO cha kiti cha ugavana Meru kimeshika kasi huku Mwakilishi wa Kike Kawira Mwangaza akizidisha kampeni zake dhidi ya gavana wa sasa Kiraitu Murungi.

Kufikia sasa, Bi Mwangaza, Mchungaji Kiambi Atheru na Waziri wa Kilimo Peter Munya, wameelezea nia yao ya kumrusha nje Bw Murungi mnamo Agosti.

Hata hivyo, ni Bi Mwangaza pekee ambaye ameanzisha kampeni zake mapema katika juhudi za kupigia debe azma yake huku akiahidi kutoa uongozi bora kupitia matumizi yanayofaa ya fedha za umma.

“Nimekuwa katika kila kona ya taifa hili na wakazi wengi wanasema hawajaona maendeleo kutoka kwa kaunti. Ndiposa nimeamua kuhamasisha watu kuhusu pesa zinazotengewa kaunti. Gavana Kiraitu amepokea zaidi ya Sh48 bilioni katika miaka minne iliyopita ambazo zinapaswa kuwajibikiwa,” alisema Bi Mwangaza wakati wa mojawapo ya mikutano yake.

“Nina hamu ya kuchukua usukani wa afisi ya gavana ili nitekeleze ndoto yangu ya matumizi bora ya fedha za kaunti.”

Licha ya kampeni zake kali, Gavana Murungi amedai mara kadhaa kuwa Bi Mwangaza hatakuwa debeni kwa sababu “hana stakabadhi zinazohitajika.”

“Bi Mwangaza kamwe si tishio kwa taaluma yangu ya kisiasa kwa sababu hana digrii. Ikiwa ni mgombea hatari, acha atuonyeshe cheti chake cha digrii. Mtu yeyote hapaswi kupoteza muda wake kwa sababu hatashiriki uchaguzi. Mpinzani hatari tu ni Waziri Munya nitakayemshinda Siku ya Uchaguzi,” alisema Bw Murungi majuzi.

Bi Mwangaza hata hivyo, amesisitiza kuwa ana shahada mbili za digrii na kumshutumu Bw Murungi kwa kuogopa ushindani.

“Gavana anapaswa kukoma kunipa vitisho na ajishughulishe kutuonyesha kazi iliyofanywa na Sh40 bilioni katika muda wa miaka minne iliyopita. Rekodi ziko wazi kuwa nina shahada ya digrii katika taaluma ya ualimu kutoka Chuo Kikuu cha Kampala na digrii ya pili katika Uongozi wa Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Pan African Christian University,” alieleza.

Bi Mwangaza, aliyejiunga na siasa 2013 kabla ya kunyakua kiti cha Mwakilishi wa Kike kwa tiketi ya mgombeaji huru mnamo 2017, ameapa kumbwaga Gavana Murungi ‘mapema asubuhi’.

“Ninatoa wito kwa wakazi wa Meru wakiwemo wataalam na watu waadilifu wanaotaka kuambatana nami katika safari kuwasiliana na mimi,” alisema.