Connect with us

General News

Kampuni za ushonaji nguo zapiga hatua kiteknolojia kilimo cha pamba kikiimarika – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kampuni za ushonaji nguo zapiga hatua kiteknolojia kilimo cha pamba kikiimarika – Taifa Leo

Kampuni za ushonaji nguo zapiga hatua kiteknolojia kilimo cha pamba kikiimarika

Na LAWRENCE ONGARO

HUKU kaunti nyingi zikipanda zao la pamba kwa wingi, kampuni za kushona nguo za jora zinaendelea kuwekeza katika mitambo inayotumia teknolojia ya kisasa.

Kutokana na hali hiyo kampuni hizo zimeonyesha ushindani mkubwa miongoni mwao.

Ukuzaji wa pamba ya aina mpya ya BT umeleta mwamko mpya kwa sababu wakulima wa pamba wamejitolea kustawisha kilimo hicho wakihimizwa na serikali waongeze juhudi zaidi.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya kushona nguo ya Thika Cloth Mills, mjini Thika, Bi Tejal Dhodhia, alisema msimamo wa kununua bidhaa za Kenya na Kujenga Kenya unaoendelezwa na kampuni hiyo umepiga hatua maradufu.

Mkurugenzi huyo alisema wakulima watazidi kupanda pamba katika maeneo yao ili waweze kuboresha maisha yao kutokana na zao hilo.

Mkurugenzi huyo aliyasema hayo alipowakaribisha wakulima wa pamba kutoka maeneo ya Malindi na Kilifi huko Pwani.

Mkurugenzi huyo alisema nchini Kenya kuna viwanda vya nguo vitatu ambavyo vimezingatia kutumia mitambo za kiteknolojia ili kushona nguo za thamani ya juu.

Alisema wakulima kote nchini wamehimizwa kupanda mbegu ya pamba aina ya BT ambayo mazao yake ni ya kutamanika. Pamba hiyo huwa ni nyeupe kabisa.

“Mashine hizo zinashona haraka na kutoa nguo za gredi nzuri zinazouzwa hata katika nchi nyingine,” alifafanua mkurugenzi huyo.

Wakulima kutoka pwani walizuru kiwanda cha Thika Cloth Mills , ambapo walijionea jinsi nguo zinavyoshonwa.

Bi Dhodhia alisema kiwanda hicho ndicho hushona nguo za watumishi wa serikali kutoka idara ya wanajeshi (KDF), kitengo cha polisi wa kupambana na ghasia (GSU), polisi, idara ya magereza na Shirika la Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS).

Ujumbe kutoka kaunti ya Meru pia ulizuru kiwanda hicho hivi majuzi ambapo pia washiriki waliridhishwa na jinsi kiwanda hicho kinavyoendesha mambo yake.

Walisema ya kwamba watawarai wakazi wa Meru kuzingatia upanzi wa pamba kwa wingi ili waweze kunufaika na zao hilo.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending