– Viongozi wa Murang’a wanataka Kenneth apewe wadhifa wa uwaziri ili kuchapa kazi serikalini
– Wadadisi wanasema hiyo ni mbinu ya kumpa ngazi kupanda kisiasa tayari kurithi eneo la Mt Kenya baada ya Uhuru kuondoka
– Wachanganuzi wamekuwa wakimuona kama mmoja wa wale ambao wanaweza kuchukua usukani wa eneo hilo kisiasa
Baadhi ya viongozi kutoka Mt Kenya wamemtaka Rais Uhuru Kenyatta kumpa aliyekuwa mbunge wa Gatanga Peter Kenneth wadhifa wa uwaziri.
Wakiongozwa na kiranja wa wengi kwenye Seneti Irungu Kang’ata, viongozi hao Jumamosi, Julai 18, walisema Kenneth ni mchapa kazi na atasaidia Rais kufunga kipindi chake kwa kazi nzuri.
Viongozi wa Murang’a wanamtaka Rais Uhuru Kenyatta kumteua Peter Kenneth kwenye baraza la mawaziri. Picha: Nation Source: UGC
“Kama Rais anapanga kufanya mageuzi kwenye baraza la mawaziri, basi ampe kazi Peter Kenneth. Tuko nyuma ya Kenneth kwa sababu tunajua atachapa kazi,” alisema Kang’ata.
Wabunge Mary Wamaua wa Maragua na mwenzake wa Gatanga Joseph Nduati waliungana na Irungu kupigia debe Kenneth.
“Viongozi wa hapa wamekubaliana Kenneth ndiye atakuwa kiongozi wetu kutoka kaunti ya Murang’a,” alisema Nduati.