Connect with us

General News

Karan Patel mawindoni kumaliza nuksi Nakuru Rally – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Karan Patel mawindoni kumaliza nuksi Nakuru Rally

Na GEOFFREY ANENE

DEREVA Karan Patel atakuwa mawindoni kuzoa ushindi wake wa pili mfululizo kwenye Mbio za Magari za Kitaifa za Kenya (KNRC) msimu huu wakati wa duru ya pili itakayofanyika kaunti ya Nakuru mnamo Machi 5.

Patel, ambaye atashirikiana na Tauseef Khan katika gari la Mitsubishi Evo10, hajawahi kushinda duru ya Nakuru licha ya kuishiriki mara tano.

Katika mashindano yaliyopita ya Nakuru, Patel alijiuzulu mwaka 2015 na 2021, akamaliza nambari sita mwaka 2017 na kukamata nafasi ya tisa mwaka 2018 na 2019.

Ataingia makala ya 2022 akiwa na motisha ya kuanza msimu kwa kunyakua taji la Kajiado Rally mwezi Januari.

Madereva wengine waliojiandikisha kuwania taji la Nakuru Rally ni Jasmeet Chana atakayeelekezwa na Ravi Chana (Mitsubishi Evo10), Issa Amwari na mwelekezi wake Job Njiru (Mitsubishi Evo10), bingwa wa Nanyuki Rally 2021 Aakif Virani atakayeshirikiana na Azhar Bhatti (Skoda Fabia).

Pia, kuna Galib Hajee/Riyaz Ismail (Mitsubishi Evo10), Hussein Malik/Deep Patel (Mitsubishi Evo10), Steve Mwangi/Dennis Mwenda (Subaru Impreza) na Daren Miranda/Amman Shah (Subaru Impreza).

Kush Patel/Mudasar Chaudry (Subaru Impreza), Rajveer Thethy/TBA (Subaru Impreza), Zameer Verjee/Zahir Shah (Subaru Impreza), Sameer Nanji/Azhar Hamid (VW Golf), Leo Varese/Kigondu Kareithi (Toyota Auris) na Sam Karangatha/TBA (Subaru Leone) wanakamilisha orodha ya washiriki. Duru hii ya kilomita 158 imedhaminiwa na kampuni ya bia ya Kenya Breweries kupitia bidhaa yake ya White Cap.

Msimamo wa KNRC 2022 baada ya Kajiado Rally:

1. Karan Patel   pointi 33

2. Jasmeet Chana  26

3. Steve Mwangi 22

4. Daren Miranda  19

5. Kush Patel  17

6. Leo Varese 15Na GEOFFREY ANENE

6. Leo Varese 15