[ad_1]
Kashfa ambazo zilipaka tope utawala wa Rais Kibaki
NA BENSON MATHEKA
INGAWA Rais Mwai Kibaki amesifiwa kwa kutekeleza mengi chini ya utawala wake wa miaka 10 ulikumbwa na kashfa ambazo pesa za mlipa ushuru ziliporwa huku akishutumiwa kwa mtindo wake wa uongozi.
Ajabu ni kwamba waliomkosoa ndio wanaomsifu kwa aliyotenda katika vipindi vyake viwili vya utawala.
Alipoapishwa rais wa tatu wa Jamhuri ya Kenya 2002 baada ya uliokuwa muungano wa NARC kushinda chama cha Kanu kwenye uchaguzi mkuu, Rais Kibaki alisema mawaziri wangewajibika kwa makosa yatakayotokea katika wizara zao.
Hii ilikuwa tofauti na mtangulizi wake Rais mstaafu Daniel Moi aliyelaumiwa na kudhibiti kila wizara chini ya utawala wake wa miaka 24.
Wanasiasa waliohudumu katika serikali ya Kanu waliokuwa katika upinzani walisema mtindo wa kuwaachia mawaziri uhuru wa kusimamia wizara zao ungetatiza utenda kazi katika serikali.
Hata hivyo licha ya shutuma hizo Rais Kibaki aliendelea kuchapa kazi na kufikia mwisho wa kipindi chake cha kwanza, waliomshtumu, akiwemo walijiunga naye kumpigia debe kwa kipindi cha pili.
Wakosoaji wa utawala wa Rais Kibaki pia walimlaumu kwa kupendelea jamii za eneo la Mlima Kenya katika uteuzi wa nyadhifa za juu serikalini.
Ingawa Kibaki aliapa kukabiliana na ufisadi katika serikali yake, utawala wake ulikubwa na kashfa zilizogharimu serikali mabilioni ya pesa.
Uchunguzi ulioendeshwa na aliyekuwa katibu wa maadili na utawala Bw John Githongo ulifichua jinsi serikali ilivyopoteza pesa nyingi kupitia kashfa ya Anglo-Leasing iliyodaiwa kuhusisha washirika wa karibu wa rais.
Baada ya kufichua kashfa hiyo Bw Githogo alitoroka nchini akidai maisha yake yalikuwa hatarini.Ahadi nyingine aliyotoa alipoapishwa ilikuwa kupitisha katiba mpya katika muda wa siku 100. Hata hivyo hilo lilifanyika baada ya miaka 8 ya utawala wake.
Next article
WANDERI KAMAU: Vyama vinavyowapunja wawaniaji vinafaa…
[ad_2]
Source link