Connect with us

General News

Kaunti zatakiwa kuanzisha mpango tamba wa utoaji chanjo – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Na CHARLES WASONGA

WIZARA ya Afya imezitaka Serikali za Kaunti kuanzisha mpango wa utoaji chanjo dhidi ya corona kwa mfumo wa kuhamahama ili kuwafikia wengi.

Kaimu Mkurugenzi wa Afya nchini Patrick Amoth, Ijumaa alisema Idara za Afya ya Umma katika kaunti zote 47 zinafaa kuendesha shughuli hiyo katika vituo vya magari, pikipiki za bodaboda, makanisani, kwenye masoko ya wazi miongoni mwa maeneo mengine ambayo hayajaorodheshwa kama vituo vya utoaji chanjo.

“Kwa kufanya hivyo, tutaweza kufikia lengo letu la kuwapa chanjo watu 10 milioni kufikia Desemba 2021. Aidha, tunakadiria kuwa ifikapo mwezi Juni 2022, jumla ya watu 30 milioni watakuwa wamepata chanjo hii,” Dkt Amoth akasema akiongea jijini Nairobi.

Mkurugenzi huyo pia aliwahimiza watu wenye umri wa miaka 50 kwenda juu kujitokeza kwa wingi kupewa chanjo akisema wao ndio wako katika hatari ya kuathiriwa na Covid-19 ikilinganishwa na watu wenye umri mdogo.

“Inavunja moyo kwamba kufikia sasa ni asilimia 10 pekee ya watu hawa wenye umri mkubwa wamepewa chanjo. Hii ni licha ya kwamba Kenya imepokea dozi nyingi za chanjo kutoka mataifa ya kigeni na mashirika mengi,” akasema Dkt Amoth.

Alisema hayo alipoongoza hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Kitaifa wa Kimkakati wa kutambua na kupambana na Milipuko ya Magonjwa. Mpango huo wa kimkakati unatoa mwongozo wa namna ya kupambana na magonjwa hayo (ikiwemo Covid-19) kote nchini. Utatumika kuanzia 2021 hadi 2026.

Hafla ya uzinduzi wa mpango huo ilifanyika Ijumaa katika Mkahawa wa Four Point Sheraton, mtaani Hurligham, Nairobi.

Kaunti zatakiwa kuanzisha mpango tamba wa utoaji chanjo – Taifa Leo
Dkt Patrick Amoth (wa tano kutoka kushoto) na maafisa wa Wizara ya Afya waonyesha wanahabari nakala za mpango wa kimkakati wa kupambana na milipuko ya maradhi. Picha/ Charles Wasonga

Kulingana na Dkt Amoth kufikia sasa Kenya imepokea jumla ya dozi 6.5 milioni za aina mbalimbali za chanjo ya kuzuia kuenea kwa Covid-19. Aina ya chanjo hizo ni pamoja na; AstraZeneca, Moderna, Pfizer, Johnson & Johnson, na Surphram kutoka China.

“Kufikia sasa tumetoa jumla ya dozi 3.5 milioni kati ya dozi zote ambazo tumepokea. Nina imani kuwa kufikia Desemba tutafikisha lengo letu la kutoa chanjo kwa angalau watu 10 milioni,” akaeleza.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending