[ad_1]
Kibaki alinisaidia kutoka uhamishoni Uganda, Rwanda – Mzee Wangamati
NA BRIAN OJAMAA
MWENYEKITI wa Baraza la Wazee wa jamii ya Waluhya Patrick Wangamati ameelezea jinsi Hayati Mwai Kibaki alivyomuokoa alipokuwa akiishi uhamishoni nchini Uganda na Rwanda.
Mbunge Maalumu huyo wa zamani wa Ford Kenya, alisema kuwa alikimbilia katika nchi hizo jirani wakati wa utawala wa Rais Daniel Moi.
Mzee Wangamati ambaye pia ni baba ya Gavana wa Bungoma Wycliffe Wangamati, alisema kuwa Rais Kibaki alimrejesha humu nchini baada ya kuishi mafichoni kwa miaka 20.
Alikuwa miongoni mwa Wakenya waliokuwa wakipinga mfumo wa chama kimoja mnamo 1992.
Bw Wangamati na wanasiasa wengine kutoka eneo la Magharibi walikuwa wameunda kundi la February Eighteenth Movement (FERA) lililokuwa likipewa mafunzo kando ya Mlima Elgon na mashariki mwa Uganda kujiandaa kukabiliana na utawala wa kidikteta wa Moi.
“Kibaki ndiye alizungumza na Rais Moi na kumshawishi aruhusu nirejee Kenya baada ya kuishi kwa miaka mingi Uganda na Rwanda,” akasema Mzee Wangamati.
Mbunge huyo wa zamani alidai kuwa maafisa wa ngazi wa juu serikalini walikuwa wameagiza auawe.
‘Tulipokuwa tukipigania mfumo wa vyama vingi nchini, kulitokea mapigano mengi ya kikabila katika maeneo mengi ya nchi. Nilipomsihi Rais Moi aniruhusu kumaliza machafuko hayo, alinitimua nchini.
“Lakini Kibaki alipoteuliwa kuwa waziri wa Fedha alimshawishi Moi kunirejesha,” akasema.
Mzee Wangamati alisema kuwa alipokuwa akiishi uhamishoni, alipata marafiki wengi na wakati mmoja alialikwa na Umoja wa Mataifa (UN) kuelezea maovu ya serikali ya Moi.
Alisema kuwa walisihi UN kukoma kufadhili serikali ya Moi kwa kukandamiza demokrasia.
Mzee Wangamati alisema Kibaki wakati huo alikuwa na ushawishi mkubwa ndani ya Kanu ambacho kilikuwa chama cha kisiasa pekee humu nchini.
[ad_2]
Source link