Connect with us

General News

Kikundi cha wanajuakali Kiambu chafurahia pendekezo la Raila – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kikundi cha wanajuakali Kiambu chafurahia pendekezo la Raila – Taifa Leo

Kikundi cha wanajuakali Kiambu chafurahia pendekezo la Raila

NA LAWRENCE ONGARO

KIKUNDI cha wanajuakali kutoka kaunti ya Kiambu, kimepongeza hatua ya kinara wa ODM Raila Odinga, ya kuahidi atawatetea iwapo atapata uongozi wa nchi Agosti 9, 2022.

Mwenyekiti ya wanajuakali mjini Thika, Bw Mwangi Kamau, alieleza kuwa watazindua kampeni kabambe kuona ya kwamba Raila anaingia ikulu, ili aweze kutetea maslahi yao.

“Kwa muda mrefu wanajuakali wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya ujenzi wa taifa lakini pesa wanazolipwa ni duni kweli,” alisikitika Bw Kamau.

Alitoa mfano wa kazi inayoweza kufanywa na kugharimu Sh100,000, lakini aliyefanya kazi hiyo ambaye ni mwanajuakali anapokea Sh3,000 pekee, huku mawakala wakibaki na kiasi kilichosalia.

Bw Kamau alisema hotuba ya Raila iliwagusa roho na imebidi wajisahili kwa makini na kufanya uamuzi wa kuwafaidi siku za usoni.

Walisema mawakala ndio wamekuwa kikwazo kikubwa katika sekta ya juakali. Bw Kamau alieleza kuwa vijana wengi wana ujuzi wa kuunganisha injini ya gari na ni sawa na ujuzi wa mwanafunzi aliye chuo kikuu.

“Iwapo Raila atazingatia ahadi hiyo bila shaka vijana wengi watanufaika pakubwa na maswala ya ajira hapa nchini,” alisema Bw Kamau.

Bi Esther Wangeci, ambaye pia ni mfanyibiashara katika sekta ya juakali alisema huu ndio wakati wa kujiamulia hatima yao ya siku zijazo.

Alisema wanajuakali wanastahili kushirikiana wote kwa pamoja na kumfanyia kampeni Raila.

Wanajuakali hao kwa pamoja walikiri ya kwamba iwapo pendekezo la Raila litafanikiwa bila shaka uchumi wa nchi utaimarika pakubwa ambapo wanajuakali popote walipo watajivunia kuwa na ujuzi kamili wa kuwanufaisha kimaisha.

Alisema wanawake walifurahia matamshi ya Raila aliposema anaelewa shida za wanawake hasa walio na biashara ndogondogo.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending