Connect with us

General News

Kimathi sasa ajiandaa kwa Croatia Rally – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kimathi sasa ajiandaa kwa Croatia Rally – Taifa Leo

Kimathi sasa ajiandaa kwa Croatia Rally

NA GEOFFREY ANENE

DEREVA McRae Kimathi, 27, anatupia jicho duru ya dunia ya Croatia baada ya kuanza kampeni ya kutetea taji la Mbio za Magari za Afrika (ARC) kitengo cha chipukizi vibaya, kwenye Equator Rally eneobunge la Naivasha mnamo Aprili 1-3.

Kimathi (pichani kulia na mwelekezi wake Mwangi Kioni) alitwaa taji la Afrika 2021 alipokamata nafasi ya kwanza katika kitengo cha chipukizi kwenye duru ya Mountain Gorilla nchini Rwanda na nambari mbili kwenye duru ya Oryx Energies Tanzania.

Jumapili, alimaliza Equator Rally 2022 katika nafasi ya nne kwenye kitengo hicho na nane kwa jumla huku Mkenya Karan Patel akinyakua taji la jumla.

Aliwafuata Jeremy Wahome, Maxine Wahome na Hamza Anwar mtawalia.

Kimathi akishirikiana na Mwangi Kioni walipoteza dakika 2:50 baada ya kusumbuliwa na gari lao la Ford Fiesta R3 katika mikondo ya Sleeping Warrior 1 na Soysambu 2.

Walifanya duru ya dunia ya Uswidi kwenye theluji mwezi uliopita na watakuwa Croatia kupaisha kwenye lami mnamo Aprili 21-24.

Aidha, Karan sasa atashiriki duru zilizosalia za Afrika (Uganda, Tanzania, Rwanda, Zambia na Afrika Kusini) kuhakikisha linasalia Kenya baada ya Carl Tundo (2021), Manvir Baryan (2017, 2018 na 2019), Don Smith (2016) na Jaspreet Chatthe (2015) kushinda makala sita yaliyopita.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending