Kimemia apuuzilia mbali madai kuwa magavana wanashurutishwa kuunga mkono Raila
Na CHARLES WASONGA
GAVANA wa Nyandarua Francis Kimemia amesisitiza kuwa magavana kutoka eneo la Mlima Kenya wanaounga mkono azma ya kiongozi wa ODM Raila Odinga ya kuwania urais wanafanya hivyo kwa hiari yao wala hawalazimishwi na serikali.
Akiongea Jumatatu, Novemba 8,2021, asubuhi kwenye kipindi cha mjadala kuhusu masuala mbalimbali nchini katika runinga ya Citizen, Bw Kimemia alipuuzilia mbali madai kuwa magavana kutoka eneo hili wanashurutishwa kuunga mkono waziri huyo mkuu wa zamani.
“Wengi wetu kama magavana kutoka Mlima Kenya tumekuwa tumekuwa tukimuunga mkono Raila kutokana na sera na maongozi anazouzia watu wetu. Tunaona kwamba sera zake zinaweza kuleta maendeleo kwa watu wetu,” Bw Kimemia akasema katika kipindi hicho kinachoongozwa na mwanahabari Sam Gituku.
Naibu Rais William Ruto na naibu wake wakuwa wakishikilia kuwa magavana kutoka Mlima Kenya wamelazimishawa na Serikali Kuu kuunga mkono azma ya urais ya Waziri huyu Mkuu wa zamani.
Seneta wa Meru Mithika Linturi ambaye pia alishiki katika kipindi hicho cha Day Break alitofautiana na kauli ya Bw Kimemia akisema viongozi wengi kutoka Mlima Kenya wanaomuunga mkono Bw Odinga wanafanya hivyo kuwa kulazimishwa na serikali.
“Mawaziri, makatibu wa wizara, magavana na maafisa wengine wakuu wanashurutishwa kumuunga mkono Raila. Hii ni kwa sababu Raila Odinga ni mradi wa serikali katika siasa hizi za urithi wa Rais Uhuru Kenyatta,” akaeleza Linturi ambaye ni Seneta wa Meru.
Linturi ambaye ni mmoja wa washirika wakuu wa Dkt Ruto kutoka eneo la Mlima Kenya Mashariki, alidai kuwa magavana ambao hutaka kugura Jubilee hutishwa kwa kuwekeza kesi za ufisadi. Hata hivyo, Bw Kimemia alikana madai hayo akisema magavana wa Mlima Kenya hawana kesi za ufisadi
“Magavana kutoka Mlima Kenya sio wanahalifu wa kuhofia kukamatwa na asasi za kupambana na ufisadi kama vile EACC, DCI na KRA. Magavana kutoka Mlima Kenya ni viongozi wenye maadili ambao hawawezi kutumia afisi zao kupora mali ya umma,” Bw Kimemia akaeleza.
Hisia hizo zinajiri siku mbili baada ya Bw Odinga kufanya ziara ya kufanya katika kaunti ya Nyandarua inayosimamiwa na Bw Kimemia ambaye alikuwa mwenyeji wake.
Bw Odinga alihutubia mikutano katika vituo kadha katika kaunti hiyo huku akiandamana na magavana Lee Kinyanjui (Nakuru), James Nyoro (Nakuru), Ndiritu Muriithi (Laikipia) miongoni mwa viongozi wengine.
Next article
Hakuna kupimwa wazimu kwa washukiwa wa mauaji