Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu ametangaza kuwa anatarajia kurejea nchini humo Julai 28, baada ya kuishi ughaibuni kwa zaidi ya miaka 3
Lissu amekuwa akipokea matibabu ughaibuni baada ya kupigwa risasi mara kadhaa na watu wasiojulikana mwaka wa 2017.
Lissu alisema wahalifu waliojaribu kumuua bado hawajakamatwa na anaamini serikali ya sasa ilihusika katika njama ya kutaka auawe.
”Hivyo ninarejea nyumbani kuikabili serikali iliyosema kuwa haina hatia katika tukio hilo la jaribio la kuniua, kunizuia kutadhihirishia dunia kuwa ilihusika na shambulio la mwaka 2017 kama nilivyosema sina sababu ya kuamini kuwa nitazuiwa kurejea nyumbani”.Lissu alisema.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.