Kijogoo kutoka eneo la Southlands mtaani Lang’ata alibaki amepandwa na mori kisura aliyemnunulia nguo maridadi na kumfanyia ‘shopping’ kudinda kumpakulia asali.
Semasema zinaarifu kwamba lofa ambaye ni mhudumu wa bobaboda amekuwa akimmezea mate dada huyo kwa siku nyingi ila mrembo alimhepa kila alipomwona.
Hata hivyo, demu hakutokea jinsi walivyokubaliana na jamaa akabaki kwenye kijibaridi akipiga simu ambazo hazikujibiwa huku akikodolea macho hasara kubwa aliyokadiria.
Siku iliyofuata aliamua kwenda kwa kidosho lakini alionacha mtema kuni kwani alifurushwa na vijana wa mtaani ambao demu aliwalipa.
“Hizi bidhaa za shilingi mbili ndizo unanidanganya kuwa zitanishawishi kulala na wewe? Shika adabu zako na utokomee mimi sio kiruka njia,” mrembo alimuonya.
Duru za mtaani humo zinasema jamaa ambaye alikuwa na hasira alijaribu kumtandika demu lakini alizuiwa na vijana waliotishia kumharibu sura.
Ilibidi barobaro aondoke akiwa amefyata mdomo baada ya kuonywa kuwa vijana hao wangemnyorosha bibaya iwapo hangeondoka mtaani
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.