Connect with us

General News

KPA kutumia Sh2m kusaidia wahanga wa njaa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

KPA kutumia Sh2m kusaidia wahanga wa njaa – Taifa Leo

KPA kutumia Sh2m kusaidia wahanga wa njaa

Na WINNIE ATIENO

HUKU janga la ukame likiendelea kuwaathiri baadhi ya wakazi wa kaunti za Lamu, Tana River, Kilifi na Taita Taveta kampuni ya Bandari nchini itatumia Sh2 milioni kutibu wahanga na baa la njaa hasa watoto wanaokabiliana na utapia mlo.

Kampuni hiyo ya KPA inalenga watu 20,000 wanaokabiliwa na ukame katika kijiji cha Chanagande kaunti ya Kilifi.

Hii leo (Jumamosi) KPA itawapa wakazi hao huduma za afya, dawa, kutibu wagonjwa na kuwapa rufaa wakazi ambao wanahaika na magonjwa sugu kama vile kisukari, saratani na shinikizo la dawa.

Magonjwa mengine yanayolengwa kwenye ni pamoja na malaria, kifua kikuu, kuendesha, magonjwa ya ngozi na ukosefu wa damu mwilini.

Wauguzi, madaktari na wataalam wa afya kutoka KPA watashirikiana na wale wa wale wa kaunti ya Kilifi wanalenga watoto ambao wanaugua maradhi ya ukosefu wa lishe bora hasa utapia mlo na marasmus.

KPA imekuwa ikihimiza uhisiano mwema kwa kutoa misaada ya afya, kuhimiza mazingira bora kwa kupanda miti hasa wakati wa majanga.

KPA pia imekuwa ikikuza talanta za vijana.