[ad_1]
TUSIJE TUKASAHAU: Kumbe ahadi ya Uhuru kustawisha uchukuzi wa majini ilikuwa hewa tu!
NA CHARLES WASONGA
MNAMO Novemba 16, 2018 Rais Uhuru Kenyatta alielezea jinsi serikali yake imejitolea kustawisha uchukuzi wa majini kama mojawapo ya njia ya kudumisha biashara na uchumi wa majini.
Alisema hayo alipofungua rasmi Kongamano la Ulimwengu kuhusu Uchumi wa Baharini katika jumba la KICC, Nairobi.
Lakini Rais Kenyatta asije akahau kwamba, utekelezaji wa ahadi hiyo katika Ziwa Victoria hautafanikiwa kufuatia hatua ya Mamlaka ya Shughuli za Majini (KMA), kupiga marufuku shughuli za feri za kibinafsi.
Wakazi pamoja na wafanyabiashara wanaohudumu kati ya mji wa Mbita hadi visiwa vya Rusinga na Mfangano, wamekuwa wakiteseka kuanzia Novemba mwaka jana kufuatia hatua hiyo.
Viongozi na wakazi wa eneo hilo, sasa wanaomba serikali inunue feri ya umma ili iweze kuwahudumia sawa na inavyofanyika katika kivuko cha Likoni, Kaunti ya Mombasa.
[ad_2]
Source link