Connect with us

General News

Kundi lapendekeza Ruto ateue Waiguru kuwa naibu wake – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kundi lapendekeza Ruto ateue Waiguru kuwa naibu wake – Taifa Leo

Kundi lapendekeza Ruto ateue Waiguru kuwa naibu wake

NA JOSEPH OPENDA

KUNDI moja la vijana wanaoegemea muungano wa Kenya Kwanza linapendekeza Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru ateuliwe kuwa mgombea mwenza wa Naibu Rais William Ruto.

Kundi hilo linalojulikana kama “Kenya Kwanza National Youth Alliance” linasema Bi Waiguru ndiye atamfaa zaidi Dkt Ruto na kumwezesha kushinda katika uchaguzi huo wa Agosti 9.

Wakiongea na wanahabari mjini Nakuru, vijana hao wanaojumuisha wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vya kadri walitaja ajenda ya Bi Waiguru ya kuimarisha masilahi ya vijana, kama sifa ambayo itamsaidia Dkt Ruto kupata kura nyingi.

Katika taarifa hiyo iliyosomwa kwa pamoja Bi Babra Juma na Joyce Anne Mwita, kundi hilo lilisema Gavana Waiguru ana ufuasi mkubwa katika eneo la Mlima Kenya na taifa la Kenya kwa ujumla.

“Tunashawishika kwamba ajenda yake inaingiliana na matakwa ya Wakenya wengi,” vijana hao wakasema.

Kwa kuwa na Naibu Rais mwanamke, vijana hao wakasema, taifa la Kenya litapiga hatua katika ndoto yake ya kufikia hitaji la kikatiba la usawa wa kijinsia.

“Tunaaamini kuwa Bi Waiguru anaweza kutumikia taifa hili vizuri kama Naibu Rais kutokana na kazi nzuri ambayo amefanya akiwa gavana wa Kirinyaga. Kabla ya hapo alidumu katika serikali kuu kama Afisa Mkuu katika Wizara ya Fedha kabla ya kuteuliwa Waziri wa Ugatuzi mnamo 2013,” akasema Bi Mwita.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending