– Matilda Njoki alikabiliwa na tuhuma za kuvunja mlango wa mpangaji wake na kuiba mali yake kutokana na deni la kodi
– Alikana mashtaka na kuiambia mahakama kwamba mpangaji wake, George Wambugu alimwachia funguo za nyumba yake
– Alisema Wambugu alikosa kulipa deni la KSh 25,000 licha ya kuahidi kufanya hivyo
Landilady kutoka mtaa wa Zimmerman, Nairobi amejikuta pabaya kwa madai ya kuvunja mlango wa mpangaji na kumuibia bidhaa zenye thamani ya KSh 153,000 kwa kukosa kulipa kodi.
Matilda Njoki Ndungu alidaiwa kuvunja mlango wa George Wambugu mnamo Julai 12 akishirikiana na wenzake ambao hawakuwa mhakamani Jumatano, Julai 15.
Matilda Njoki Ndungu alipowasili mahakamani Jumatano, Julai 15. Picha: Daily Nation. Source: UGC
Mbele ya hakimu Heston Nyaga katika mahakama ya Makadara, Njoki alikana mashtaka na kusema Wambugu alimwachia ufunguo wa nyumba kulingana na Daily Nation.
Njoki aliiambia mahakama Wambugu alikuwa na deni lake la KSh 25,000 la kodi ya nyumba na alikuwa ametoweka kwa siku kadhaa kusaka pesa ila aliporudi alikuwa na KSh 2,000.