Waziri Mutahi Kagwe. Kagwe alisema serikali imewaajiri madaktari 20 kutoka Cuba kwa ajili ya Covid-19. Picha: MoH Source: Facebook
Kagwe alisema uamuzi huo umeafikiwa ili sekta ya afya ipate wataalamu wakati ambapo maradhi hayo yanaonekana kuongezeka humu nchini.
Kagwe alisema madaktari hao watafika humu nchini Alhamisi, Julai 23 na kupelekwa katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.
“Madaktari hao watafanya kazi na wale wetu ili kubadilishana ujuzi. Kuanzia 2018, tumekuwa tukifanya kazi na serikali ya Cuba na ushirikiano huo umewezesha madaktari wetu kupata mafunzo Cuba,” alisema Kagwe.
Waziri Mutahi Kagwe alisema Rais Uhuru Kenyatta alimpigia simu mwenzake wa Cuba na kukubaliana kuhusu ushirikiano katika sekta ya Afya. Picha: State House Source: Twitter
Visa vya maambukizi ya coronavirus vinazidi kuongezeka na Ijumaa vilifikia 12,062 baada ya watu 389 kupatwa na virusi hivyo.
Aidha watu watano waliripotiwa kufariki na kufikisha idadi ya walioangamia kuwa 222.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.