Magazeti haya pia yameangazia mtazamo wa viongozi wa kidini kuhusiana na hatua ya Rais Uhuru Kenyatta ya kuongezea muda Jopo Kazi la Maridhiano (BBI) na masaibu ya Gavana wa Nairobi Mike Sonko.
Kulingana na gazeti hili, huku madiwani wa Kaunti ya Nairobi wakitishia kumbandua Gavana Sonko mamlakani, imeibuka kuwa viongozi wengi wanaomugemea Naibu wa Rais William Ruto na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka wameapa kulemaza mipango yoyote ya kumtimua gavana huyo ofisini.
Wandani wa Ruto na Kalonzo kutoka Bunge la Kitaifa na Seneti wanashikilia kuwa endapo mswada huo utawasilishwa kwao, basi watatumia mbinu zote kuisambaratisha.
Haya yanajiri huku Kiongozi wa Wengi Seneti Kipchumba Murkomen, Kiranja wa Wachache Mutula Kilonzo na Mbunge wa Makueni Dan Maanzo kufika kortini kama mawakili wa Sonko.
Viongozi wengine walionyesha kusimama na Sonko ni pamoja na Mbunge Babu Owino (Embakasi Mashariki), Nimrod Mbai (Kitui Mashariki), Patrick Makau (Mavoko), Oscar Sudi (Kapsaret) Maseneta Samson Cheragei (Nandi) na Aaron Cheruiyot (Kericho).
2. Taifa Leo
Gazeti hili linaripoti kuwa baadhi ya wamiliki wa matatu kutoka eneo la Pwani wameamua kukimbilia uchawi ili kuimarisha biashara yao
Kulingana na gazeti hili, baadhi ya mapasta katika biashara hiyo ni picha tu kwani huwa wanatumia juju.
Gazeti la Taifa Leo Jumatatu, Desemba 16. Picha: Taifa Leo Source: UGC
3. Daily Nation
Gavana anayezingirwa na utata Mike Sonko anaoenekana bado masaibu yake yanaongezeka, hususan endapo Tume ya Kupambana na Ufisadi Nchini (EACC) ikiamua kumulika mali yake.
Daily Nation inaripoti kuwa, hatua ya EACC, huenda ikalenga makazi ya kifahari ya Sonko yakiwemo ya Diani, Upperhill, Greenspan, Machakos, Buru Buru na Nyari jijini Nairobi.
Gavana huyo pia anamiliki vituo sita vya burudani ikiwemo Club Volume, Club Wakanda, Casaurina, Kimeremeta, Sonko na Family resort na Salama Maridadi.
Mali nyingine inayomilikiwa na Sonko ni pamoja na magari 24 yakiwemo yakuzima moto na kubeba maji.
Sonko pia anamiliki vipande vya ardhi eneo la Shanzu na Kwale.
Gazeti la Daily Nation Jumatatu, Desemba 16. Picha: Nation Source: UGC
4. The Star
Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji atafika mahakamani siku ya Jumatatu, Desemba 16 kuwasilisha ombi la kufutiliwa mbali kwa dhamana ya Gavana wa Samburu Moses Lenolkulal.
Kulingana na DPP, Lenolkulal alikiuka masharti ya dhamana hiyo kwa kufanyia mabadiliko baraza la mawaziri.
Haji anasema haya yatatatiza ushahidi.
Endapo mahakama itafuta dhamana ya kiongozi huyo wa Samburu basi inamaanisha kuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko pia hatakuwa na uwezo wa kumteua naibu gavana wake wakati huu.
Hii basi inamuacha na chaguo la kujiuzulu, kubanduliwa ama Rais Uhuru Kenyatta kufutilia mbali serikali ya kaunti hiyo endapo gatuzi hiyo itakuwa inakumbana na hatari ya kukosa kiongozi.
Gazeti la The Star,Jumatatu, Desemba 16. Picha: The Star Source: UGC
5. The Standard
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imeanzisha mchakato wa kuangazia upya mipaka ya mabunge nchini.
Zoezi hilo linatazamiwa kushuhudia baadhi ya maeneo bunge yakifutwa na mengine kubuniwa kufuatia matokeo ya sensa yaliyotolewa na Taasisi ya Unakili wa Takwimu Nchini (KNBS).
Kulingana na gazeti hili, mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chubukati ameandikia KNBS barua kuomba taarifa katika makata jambo ambalo halikuzingatiwa awali.
Hata hivyo, zoezi hilo limekumbatiwa kama njia ya kuwazima wabunge ambao maeneo yao yamo hatarini hususan eneo la Kaskazini Mashariki ambao walitishia kuenda mahakamani kupinga matokeo ya sensa ya mwaka huu.
Gazeti la The Standard, Jumatatu, Desemba 16. Picha: Standard. Source: UGC