[ad_1]
TUSIJE TUKASAHAU: Magoha ahakikishe wizara inatekeleza CBC kwa kushirikisha wadau na umma kwa ujumla
MNAMO Mei 17, 2019 Waziri wa Elimu George Magoha alitangaza kuwa Wizara yake ingeendelea kuandaa mikutano ya mashauri na wadau kujadili changamoto ibuka katika utekelezaji wa mtaala mpya wa masomo wa CBC.
Lakini mnamo Jumatatu wiki hii ilibainika kuwa Profesa Magoha hajatimiza ahadi hiyo.
Hii ni baada ya vyama vya kutetea masilahi ya walimu, Knut na Kuppet kulalamikia kutengwa katika maandalizi ya utekelezaji wa mtaala huo katika ngazi ya Gredi 6 na “Junior Secondary”. Vyama hivyo vilisema Wizara ya Elimu haijaandaa kongamano lolote kujadili suala hilo muhimu.
Waziri Profesa Magoha asije akasahau kwamba ni kinyume cha hitaji la kipengele cha 118 cha Katiba kwa asasi yoyote ya serikali kutekeleza miradi au mpango wowote pasina kushirikisha wadau na umma kwa ujumla.
Kwa hivyo, ili kutatua changamoto kadhaa zinazokumba utekelezaji wa mtaala, sharti Waziri Magoha ashirikishe wadau.
Next article
Presha kwa Ruto na Raila kuhusu wagombea wenza
[ad_2]
Source link