Connect with us

General News

Magoha ataka usajili wa upesi wa watahiniwa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Magoha ataka usajili wa upesi wa watahiniwa – Taifa Leo

Magoha ataka usajili wa upesi wa watahiniwa

NA SHABAN MAKOKHA

WAZIRI wa Elimu Profesa George Magoha ametaka usajili wa watahiniwa wote mitihani ya kitaifa uharakishwe kabla Mei 14 utakapofungwa akionya walimu watakaokosa kusajili wanafunzi kwa kutomaliza karo watachukuliwa hatua.

Prof Magoha alisema muda hautaongezwa na serikali ingependa kujua ni wanafunzi wangapi watakuwa wakifanya mitihani yao ili mipango ianze mapema.

Mwaka huu, mitihani mitatu ya kitaifa inatarajiwa kufanywa huku serikali iking’ang’ana kurekebisha kalenda ya masomo ambayo itaanzia Januari 2023.

Akiizuru shule kwenye kaunti ya Kakamega, Magoha aliwaonya wakuu wa shule akisema itakuwa kosa la uhalifu kutosajili wanafunzi ambao hawajamaliza kulipa karo.