[ad_1]
Mahakama yaamuru Sudi awasilishe hati za Uturuki
NA RICHARD MUNGUTI
MBUNGE wa Kapseret Oscar Sudi alikosa kufika kortini Jumatano ameagizwa awasilishe stakabadhi kuthibitisha alisafiri Uturuki kupokea matibabu ya dharura.
Akitoa agizo hilo hakimu mkuu mahakama ya kuamua kesi za ufisadi Felix Kombo alisema “lazima mahakama iridhike Sudi anayeshtakiwa kwa kughushi vyeti vya masomo alikuwa amesafiri la sivyo dhamana aliyopewa itafutiliwa mbali na kusukumwa gerezani.”
Hii ni mara ya pili kwa Sudi kutofika kortini.
Mnamo Machi 21, 2022 Sudi alikosa kufika kortini akidai ameambukizwa ugonjwa wa Covid-19 na aliagizwa na madaktari ajitenge na watu.
Na wakati huo huo Bw Kombo alikataa ombi la kuahirisha kesi hiyo dhidi ya Sudi akisema imekaa kortini kwa muda wa miaka sita sasa.
Bw Kombo alisema Jaji Mkuu Martha Koome ameagiza kesi zote za zamani zikamilishwe mwaka huu.
“Hii kesi dhidi ya Sudi ni mojawapo ya kesi zilizokaa kortini kwa muda mrefu tangu 2016,” Bw Kombo alisema.
Bw Kombo aliwaagiza mawakili Thomas Ruto, Collins Kiprono na George Wajakoyah wawasiliane na Sudi akiwa Uturuki kesi iendelee Mei 19 kama hayuko kortini.
Awali mawakili hao waliwasilisha stakabadhi kuonyesha mshtakiwa yuko Uturuki lakini hakimu akaeleza kutoridhika kwake.
Next article
KAULI YA WALLAH BIN WALLAH: Kamwe huwezi kufanikiwa…
[ad_2]
Source link