Connect with us

General News

Mahakama yatimua kampuni ya Uganda kutoka Mumias Sugar – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mahakama yatimua kampuni ya Uganda kutoka Mumias Sugar – Taifa Leo

Mahakama yatimua kampuni ya Uganda kutoka Mumias Sugar

Na RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA Kuu jana ilitimua kampuni ya Uganda iliyoteuliwa kufufua kampuni ya sukari ya Mumias (MSC).

Na wakati huo huo Jaji Alfred Mabeya alimtimua Ramana Rao kutoka usimamizi wa MSC.

Badala yake, alimteua Kereto Marima kuchukua mahala pake na kumwamuru afufue kiwanda hicho.

Bw Marima aliagizwa afanywe mkutano na wadeni wote wa MSC kutathmini kiwango kinachodaiwa kampuni hiyo ya kutengeneza sukari.

Bw Rao aliondolewa kwa sababu alishindwa kusimamia MSC kwa mujibu wa sheria na maagizo ya mahakama.

Jaji Mabeya alisema Rao alikaidi sheria za ufufuzi wa kampuni iliyokuwa imewekwa chini ya mrasibu wa mahakama.

“Rao alikaidi sheria za usimamizi wa kampuni iliyofilisika kwa kushindwa kuwatambua wadeni na kufanya mkutano nao kutathmini madeni yaliyofanya MSC kufilisika ,” alisema Jaji Mabeya.

Kwa mfano, Jaji Mabeya alisema kati ya 2018 na 2021 wakati Bw Rao aliteuliwa kusimamia MSC na Benki ya Kenya Commercial Bank (KCB), alikusanya zaidi ya Sh800,000,000 na hakulipa hata deni moja.

“Bw Rao alikusanya zaidi ya Sh800m na hakulipa madeni. Badala yake alizitumia pesa hizo kufanya matangazo na kutoa misaada. KCB ilifurahia kazi hiyo na kumuongezea tena Sh200milioni kuendelea na ufujaji wa pesa za umma,”alisema Jaji Mabeya.

Jaji huyo alisema MSC inadaiwa zaidi ya Sh30 bilioni.