– Samuel Mburu alimrai afisa huyo aabiri gari lake lakini alidinda na kuingia gari lingine
– Makanga huyo alipandwa na hasira na akaanza kumdhulumu
– Afisa huyo alipiga ripoti na ndiposa mshukiwa akakamatwa siku tatu baadaye
Makanga anayehudumu katika barabara ya Uthiru- Nairobi ameshtakiwa kwa dhuluma baada ya kumgusa titi afisa wa polisi.
Hakimu mkaazi wa mahakama ya Kibra Renee Kitagwa aliarifiwa kwamba mwathiriwa alipanda matatu katika kituo cha Uthiru mnamo Julai 3 wakati Samuel Mburu alimdhulumu.
Samuel Mburu aliachiliwa kwa dhamana baada ya kumdhulumu afisa wa polisi wa kike. Picha: The Standard. Source: UGC
Mahakama iliarifiwa kuwa kulikuwepo na mzozano kati ya wawili hao baada ya Mburu kumrai afisa huyo kupanda gari lake lakini aliamua kuabiri matatu nyingine.
Mwathiriwa alisema makanga huyo aliingiwa na hasira na ndiposa akamshika titi lake na kuanza kumdhulumu hadharani.