Rais Uhuru Kenyatta ameamrisha kufunguliwa kwa maeneo ya kuabudia nchini kufuatia mikakati iliyowekwa na Baraza la Madhehebu mbalimbali ya kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.

Baraza hilo lililopewa muda wa wiki tatu kukusanya maoni ya watu na kutoa ushauri wa jinsi ya kufunguliwa kwa maeneo hayo tayari limetoa mwongozo wake na ripoti kamili inatazwamiwa kutolewa kwa umma.
Akilihotubia taifa Jumatatu, Julai 6, rais alisema maeneo ya kuabudia yatarejelea huduma lakini chini ya masharti makali.

Maeneo ya kuabudia yalifungwa mnamo Machi 2020 mara baada ya kuripotiwa virusi vya corona nchini.
Alisema, watu 100 pekee ndio watakaoruhusiwa kuingia kwa wakati mmoja kufanya ibada kwa saa moja, na kwamba watu wenye matatizo ya kiafya hawatoruhusiwa katika maeneo hayo.
Vilevile Uhuru alisema, shule za kufundishia dini makanisani na Madrassas zitaendelea kufungwa.
Pia rasi alisema watakaoruhusiwa kanisai na misikitini ni wenye umri wa miaka iliyozidi 13 na wasiozidi miaka 58.