-Mama yake mshukiwa alikuwa ameripoti kwa polisi kuhusu kutoweka kwa mjukuu wake eneo la Elementaita
– Mama huyo anadaiwa kumuuzia mama mwingine mtoto wake wa miaka saba kwa KSh14,000 eneo la Kisii
– Bado haijabainika bayana chanzo cha Kemunto kuamua kumlangua mwanawe.
Mama mmoja aliyeshutumiwa kwa kumuuzia mama mwingine eneo la Kisii mtoto wake wa kiume mwenye miaka saba kwa KSh14,000, amekamatwa.
Irene Kemunto,ambaye ndiye mama mzazi wa mtoto huyo aliyelanguliwa kutoka Elementaita, Kaunti ya Nakuru, alikamatwa eneo la Nyansiongo pamoja na mama mwingine aliyetambuliwa kama Ziporah Nyabate.
Nyabate anadaiwa kumnunua mtoto huyo kwa KSh13,800 na alikamatwa nyumbani kwake mjini Kisii ambapo mtoto huyo alipatikana, kama ilivyoripoti gazeti la The Standard.
Kulingana na Kamishna wa Polisi Kaunti ya Nyamira, Amos Mariba, mama yake Kemunto alikuwa amepiga ripoti kuhusu kutoweka kwa mjukuu wake katika Kituo cha Polisi cha Elementaita mnamo Alhamisi, Juni 18.
Wawili hao walikamatwa eneo la Nyansiongo, Kisii. Picha: UGC. Source: UGC