Akithibitisha kisa hicho, Kamanda Mkuu wa Polisi wa Nyando, Leonard Matete alieleza kuwa walifahamishwa na baba mkwe wa Atieno kuhusu tukio hilo ambalo lilitokea wakati marehemu alikuwa amekuenda kuchukua samaki wa kupeleka sokoni.
Matete alieleza kuwa wakati alifikia friji hiyo, tochi ya mlango wake ulimpiga papo hapo na kisha Atieno alianza kupiga kamsa kabla ya kuanguka sakafuni, kama ilivyoripoti The Standard.
Atieno alipigwa na tochi ya mlango wa friji. Pich:IKEA. Source: UGC
Atieno aliaga dunia alipokuwa akikimbizwa katika Hospitali ya Boya na baadaye mwili wake kupelekwa katika makafani ya Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Ahero.
Matete alitaja tukio hilo kama lisilokuwa la kawaida na kuitaka Kampuni ya Kusambaza Umeme Nchini iwasaidie katika uchunguzi kuhusu suala hilo.
Kifo chake kinakujia miezi sita baada ya marehemu mume wake William Omondi almaarufu Sisqo, kuaga dunia mnamo Novemba 2019 katika mauaji ya kinyama eneo laBusia.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.