Connect with us

General News

Mama awadunga wanawe kisu, mmoja afariki – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mama awadunga wanawe kisu, mmoja afariki – Taifa Leo

Mama awadunga wanawe kisu, mmoja afariki

Na WANGU KANURI

MAMA mmoja katika kijiji cha Kianjogu, Kaunti ya Murang’a anasakwa kwa kuwadunga kisu watoto wake wawili ambapo mmoja alifariki papo hapo, Jumapili jioni.

Nancy Munjiro, 21, aliwavamia na kuwadunga kisu watoto wake wa kiume wenye umri wa miaka miwili na minne, nyumbani kwa nyanya yao kabla ya yeye kujaribu kujitoa uhai.

Akithibitisha kisa hicho, Naibu Chifu wa eneo hilo Bi Lucy Muthoni Kimani alieleza Idara ya Upelelezi (DCI) kuwa Bi Munjiro alikuwa akifanya kazi ya ujakazi katika eneo la Kiriaini na alikuwa amemtembelea mamake, ambaye alikuwa akiishi na watoto hao, kwa sherehe za sikukuu.

Hali kadhalika, Bi Munjiro alikuwa anapaswa kurejea kazini lakini akachelea kwa sababu zisizojulikana.

Jumapili hiyo, mamake Munjiro alikuwa ameondoka asubuhi lakini aliporejea, aliwapata wajukuu wake wakiwa wamelowa kwa damu sakafuni.

Polisi waliofika huko walipata kamba ikining’inia kwenye paa la nyumba huku ikidaiwa Bi Munjiro alijaribu kujitia kitanzi lakini akaamua kutoroka.

Mtoto huyo wa umri wa miaka minne alikuwa na pigo hafifu na akapelekwa katika hospitali ya Muriranjas kwa huduma ya kwanza. Baadaye alipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Murang’a hali yake ikiwa mbaya.