-Mwanamke huyo anasemekana alikuwa amekodisha nyumba hatua chache kutoka mahali ambapo Lali na Muigai walikuwa wanaishi
-Lali alisafiri kuelekea Lamu punde baada ya Mholanzi huyo kurejea Pwani akitokea likizo mjini Naivasha
– Mwanamke huyo anadaiwa kujaliwa mtoto mmoja pamoja na Lali
Makachero wanaochunguza kifo tatanishi cha marehemu binti ya wamiliki waKampuni ya Pombe na Mvinyo ya Keroche, Tecra Muigaisasa wanadai kuwa mpenzi wake Omari Lali alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mwanamke Mholanzi.
Mwanamke huyo ambaye alijaliwa mtoto mmoja pamoja na Lali, anasemekana alikuwa amekodisha nyumba kilomita sita kutoka mahali ambapo Lali na Muigai walikuwa wanaishi.
Huenda makachero sasa wakatumia kutumia mbinu tofauti katika kesi hiyo baada ya ripoti ya upasuaji kuzua shaka katika madai kuwa kuanguka kwa Tecra kutoka kwa ngazi za nyumba ndio chanzo cha kifo chake.
Tecra alifariki mnamo Mei 2, 2020, katika eneo la Shella, Kisiwa cha Lamu, baada ya kuanguka katika nyumba walimokuwa wakiishi pamoja na mshukiwa mkuu.
Tecra alifariki mnamo Mei 2, 2020, akipokea matibabu hospitalini.Picha:UGC. Source: UGC
Kulingana na mwanapatholijia wa serikali, Johansen Oduor, upasuaji uliofanywa kwenye mwili wa Tecra ulionyesha alikuwa na majeraha kwenye kichwa ambayo sio ya kuangua kutoka ngazi za nyumba.
Ripoti hiyo pia ilitambua kwamba marehemu hakuwa amebugia pombe kama ilivyodaiwa awali.
Mlinzi wa nyumba ambayo Tecra alianguka aliwaambia wapelelezi kuwa Lali aliwaagiza kupanguza damu iliyotokana na ajali ndogo.
Haya yanajiri siku chache baada ya Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) kumuondolea Lali mashtaka ya mauaji.
Upande wa mashtaka ulifikia uamuzi huo dhidi ya mshtakiwa kwa kutaka uchunguzi.uanzishwe siku moja baada ya mahakama kuagiza Lali apimwe akili.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.