Connect with us

General News

Mapenzi kwao basi! – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mapenzi kwao basi! – Taifa Leo

Mapenzi kwao basi!

NA SINDA MATIKO

MIAKA mingi imepita -saba hivi nafikiri, Diamond Platnumz alipoingia studio na kutunga wimbo Mapenzi Basi. Ngoma ilikuwa hiti licha ya kuwa hakuitolea video. Moja kati ya mishororo kwenye wembe huo, jamaa aliimba…

“Haya mapenzi basi, hayana maana, yalinifanya mi nichekwe…” Kipindi hiki kilimkuta msela akiwa amezenguana na mpenzi wake wa muda mrefu Wema Sepetu.

Wiki iliyopita, Diamond aliachia EP yake First of All (FOA). Kwenye moja ya ngoma, anakiri kuwa yeye ni kicheche. Kamwe hawezi kutulia na mwanamke mmoja. Hawezi kabisa kuwa mwaminifu kwa mwanamke mmoja. Inawezekana Zuchu hana shaka na hili, si wajua tena dini inamruhusu. Kimsingi mapenzi kwa mwanamke mmoja kwa Diamond ndio hapana.

Lakini sio yeye tu, mwigizaji mzalendo mwenzake Farida Kajala, Ex wake Harmonize, naye kaibuka na kusema kachoshwa na mapenzi hivyo kaamua kukaa singo sababu yeye akipenda, hupenda kwa juhudi na nguvu nyingi sana. Na kwa mtazamo wake, tatizo la kizazi cha sasa ni kwamba hakidhamini tena penzi la aina hiyo.

Unaweza ukashindwa kumwelewa Kajala mwenye miaka 41. Kama alishindwa kupata penzi hilo na watu wa kizazi chake, alitegemea iwe tofauti na kizazi hiki? Ila hiyo sio mada. Kwa ujumla penzi limeondokea kuwa mzigo kwa mastaa wengi. Ukiachana na Kajala aliyeamua kukaa singo baada ya mapenzi kumlemea, pia kunao hawa;

CORAZON KWAMBOKA

Soshiolaiti huyu naye alivuruga sana. Lakini katika haya maisha kila kitu huwa na wakati wake.

Kwa sasa toka awe mama, ni vigumu kusema ni soshiolaiti sababu kaonyesha kupunguza mapepe aliyokuwa nayo.

Mwenyewe baada ya kushtumiwa kumwiba mume wa mtu, alitangaza kuachana na mpenzi wake Frankie Just Gym It mwezi uliopita. Alisema ameamua kujipa kipau mbele. Juzi kasema kwa sasa anaugua sonona na anapambana kuwa sawa pamoja na kuendelea kuenzi maisha ya usingo. Unaweza kuongeza moja na moja ukaona hali hii huenda imesababishwa na nini. Maureen Waititu aliugua sonona baada ya Frankie kumtema lakini sasa maisha yake ni tofauti.

Hivi majuzi staa wa Bongo Movie, Farida Kajala kakiri wazi kuchoshwa na mapenzi, mzigo unaozidi kuwalemea wenzake kibao

OTILE BROWN

Staa huyu kavuruga sana hii mitaa akitoka na wanawake kadhaa akiwemo soshiolaiti Vera Sidika. Ila uhusiano wake ulioonekana kumteka yeye na mashabiki wake ni alipokuwa na mrembo kutoka Ethiopia, Nabayet.

Utakumbuka penzi lao lilikuwa nzito kiasi cha jamaa kusafiri mara kwa mara kumcheki mrembo wake. Penzi lilikuwa tamu hadi jamaa akatoa wimbo Nabayet akimsifia mtoto wa watu. Lakini lilikumbwa na misukosuko kibao.

Mapema mwaka huu walijaribu tena kulifufua kwa Nabayet kusafiri kuja Kenya. Ila baada ya kushindikana, kila mmoja aliamua kushika hamsini zake. Sasa Otile kasema ameamua kukaa singo. “Nipo singo na sina pupa. Hicho ndicho kitu watu hawaelewi. Hapa nilipofikia nimeamua kutulia nichukue muda wangu. Nimegundua kuwa watu wanaogopa kuwa singo, kila mtu anataka aonekane na mtu. Lak- ini dunia ya sasa ina ubaya,” bra- tha kaka anasema.

BRENDA WAIRIMU

Kweli wanasema binadamu ni bora katika kupanga ila mpangaji bora ni Mungu. Hivi ni nani hakutegemea kuwa mwigizaji huyu angeishia kuwa mke wa rapa Juliani? Baada ya penzi la miaka minane na misukosuko yote waliyokumbana nayo, hatimaye waliachana kabisa. Msela wa rasta akakutana na aliyekuwa mpenzi wake Gavana wa Machakos Alfred Mutua, na ndani ya mwaka mmoja, wakaoana. Kweli kilichoandikwa ndicho hutimia.

Kutoka hapo Wairimu aliamua kuishi solo akimlea binti yao.

Aliamua hata kuhama kutoka Nairobi na kwenda kuishi Mombasa alikozaliwa na kulelewa. Mwenyewe amekiri, bado anajifunza kudeti tena sababu baada ya kuumizwa sana mtima na kuvunjika kwa penzi lake na Juliani, aliamua kukaa singo. Sasa ukimwona kama yupo kwenye mahusiano, inawezekana ikawa ni kwenye filamu.

DADDY OWEN

Toka ile drama iliyomkuta miaka miwili iliyopita anayodaiwa kukimbiwa na mke wake wa zaidi ya miaka mitatu Faridah Wambui, hali yake imekuwa mbaya sana. Aliugua sonona na hata kupelekea muziki wake kushuka. Sijui mara yako ya mwisho kusikia hiti kutoka kwake ilikuwa lini? Tangu wakati huo ameishi maisha ya upweke. Kwa sasa ameshaizoea hali hiyo na anasema, hana haraka tena kuwa kwenye mahusiano. “Watu wanauliza kama ninadeti tena, kama ninapanga kuona tena. Jibu langu ni, hapana! Kwa nini? Nahisi unapovunjwa moyo kwa kiasi kama kile, hukufanya kubeba mzigo mzito wa hisia kwa muda na hii inaweza kuwa hatari katika mahusiano mapya. Katika hali kama hii, unamwachia Mungu akuongoze,” aliwahi kusema hivi karibuni.

BETTY KYALLO

Kuna kipindi maisha yake hayakuwa yakifuatiliwa sana alipokuwa mtangazaji wa TV. Ila alipoamua kuachana na utangazaji, watu walianza kupata kumjua Betty kivingine. Alianza kuyaanika maisha yake.

Toka ndoa yake kwa mwanahabari mwenza Dennis Okari kuvunjika baada ya miezi sita tu, mrembo huyo kavumishwa kutoka na wanaume kadhaa akiwemo Gavana mmoja wa Pwani, Somali bae, wakili Nick Ndeda anayedaiwa kurudiana naye miongoni mwa madume mengine.

Lakini juzi msupa huyo alisema ameamua kukaa singo huku akisisitiza kuwa hajutii watu aliowahi kutoka nao. “Wajua kwenye mapenzi huwezi kuchagua utakayempenda. Kwa sasa nimeamua kuishi maisha haya ya kuwa solo. Nafurahia nafasi hii niliyo nayo ya kuwa singo. Ndio kuna wanaume wanaonifukuzia lakini kwa sasa acha nikae hivi. Nimegundua nimekuwa nikitumia nguvu nyingi sana kupenda. Sasa nataka kuelekeza nguvu hizo kwenye biashara zangu,” alitamka.