Marafiki wake Burale walisema anaendelea kupata nafiuu akiwa nyumbani kwake mtaani Karen.
Aidha ripoti za kuugua kwake zilikuwa zimetiliwa shaka na baadhi ya wanamtandao lakini rafiki yake mmoja aliwata Wakenya kujilinda dhidi ya virusi hivyo.
Mhubiri mwenzake Karol Tunduli alidhibitisha kuwa Burale yuko nyumbani akisema wanafurahia kupona kwake.
“Sasa tunaweza kucheka jinsi waziri wa Afya Mutahi Kagwe alikupa jina lipya alipokuita Roberth Murathe. Karibu nyumbani. Tutaishi kumshukuru kwa ushindi wako Robert Burale,” alisema Tunduli.
“Nilifanyiwa ukaguzi na kupatikana na Covid-19 saa 24 baadaye. Dakatari aliingia katika chumba nilichowekwa na kuniarifu nimepatikana na virusi hivyo na kwa hivyo siwezi kuenda nyumbani,” alisema.
Wakenya hata hivyo walishuku hali yake baada ya kuwa akipeperusha hali yake kwenye mitandao hadi akiwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.