Ngunjiri Wambugu alisema kuna watu wanataka kujinufaisha na mamlaka ya Rais Uhuru Kenyatta. Picha: Standard Source: Facebook
Mbunge wa Nyeri Mjini Ngunjiri Wambugu, ambaye alianzisha mrengo wa Kieleweke, amesema kuna watu wanataka kujinufaisha na mamlaka ya Rais.
Wambugu alisema kwa sasa kuna vikundi viwili ndani ya mrengo wa serikali, ‘DealMakers na GateKeepers’.
“Kila mfalme ana vikundi hivi viwili, GateKeepers ni watu ambao humfanyia kazi na kuhakikisha wanamlinda na kulinda kazi yake. DealMakers nao ni marafiki wake wa awali kabla awe mfalme. Huwa wanataka kujinufaisha na mamlaka yake kwa ajili ya maslahi yao binafsi,” alisema Ngunjiri.
Rais Uhuru Kenyatta. Kenyatta amekuwa akiwapiga teke wandani wa DP Ruto ndani ya Jubilee akisaidiwa na mrengo wa Kieleweke. Picha: State House Source: Facebook
“Wakati mwingi, vikundi hivi viwili huwa linazozana. Katika siku zijazo, nitakuwa nikielezea nani ni nani,” mbunge huyo aliongeza.
Ngunjiri alisema sabbau ya kuanzisha Kieleweke ilikuwa ni kuhakikisha kuwa mamlaka yako kwa Rais pekee lakini sasa kuna marafiki wanaotumia nafasi yao vibaya.
“Mamlaka huwa na mtu mmoja tu. Hayawezi kuwa na watu wawili, hata kama ni marafiki,” alisema.
Naibu mwenyekiti wa Jubilee David Murathe ni mmoja wa wandani wa Rais Uhuru Kenyatta tangu walipokuwa shuleni. Picha: State House Source: Facebook
Tayari Ngunjiri amemkosoa naibu mwenyekiti wa Jubilee David Murathe kwa matamshi yake kuhusu chama cha ODM na matakwa yake ya kuhusisha kwenye kamati za bunge.
Alimtaja Murathe kama mtu asiye na shukrani kwa waliomsaidia katika kuvuka mto mkubwa.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.