Connect with us

General News

Mashindano ya kusoma Kurani yawapa fursa kuzuru Mecca – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mashindano ya kusoma Kurani yawapa fursa kuzuru Mecca – Taifa Leo

Mashindano ya kusoma Kurani yawapa fursa kuzuru Mecca

NA ABDULRAHMAN SHERIFF

MOJAWAPO ya mambo makuu ambayo Waislamu kote ulimwenguni hupenda kuyafanya mwezi wa Ramadhani, ni kuwahusisha watoto na vijana katika mashindano ya kukariri Kuran.

Mashindano hayo hufanyika kwa karibu kila nchi ya Kiislamu; wanaoshin – dana huanzia sehemu ya maandiko na kuendelea bila kuwa na mahali pa kusoma.

Kwa njia hiyo, huwaimarisha kifikra na kiroho, kuweza kuyahifadhi maneno ya Mwenyezi Mungu rohoni.

Jijini Mombasa, kijana Mohammad Ahmad Mohammad wa Chuo cha Tahfidh Bani Swaqr, alifanikiwa kupata zawadi ya kwenda Mecca, Saudi Arabia, kufanya Umra.

Aliibuka mshindi katika fainali ya mashindano ya kuhifadhi Kuran ya juzuu 30 iliyofanyika uwanja wa shule ya msingi ya Mvita.

Mohammad ananuia kutumia zawadi hiyo kama ilivyokusudiwa kwenda kufanya Umrah huko Mecca.

Alifurahi jinsi jitihada zake za kuhifadhi Kuran zimemsaidia kutimiza lengo alilokuwa nalo la kwenda huko sehemu takatifu.

“Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia kushinda mashindano haya, ambayo zawadi niliyoipata ni kubwa ya kwenda kufanya Umrah.

“Japo nimeambiwa nikitaka pesa nitapewa Sh180,000 lakini nimeamua kutumia zawadi hiyo kama ilivyokusudiwa,” akasema kijana huyo mwenye umri wa miaka 22.

Mashindano hayo yaliyo – husisha wanafunzi 18 kutoka madrassa tisa pamoja na wavulana na wasichana 12 wa kibinafsi.

Mwanafunzi mwingine wa chuo cha Tahfidh Bani Swaqr, Abdulrahman Musa, alishinda zawadi ya pesa taslimu Sh50,000.

Mbali na pesa hizo, Musa, 11, amefanikiwa kuchaguliwa kwenda Dar es Salaam nchini Tanzania kuwakilisha Kenya kwenye mashindano ya Kuhifadhi Kuran ya Afrika Mashariki, yatakayofanyika baadaye mwezi huu.

Mwalimu Mkuu wa chuo hicho, Haitham Swaqr, alisema kuwa atamsindikiza Musa kwenye safari hiyo ya Tanzania akiwa na matumaini ya mwanafunzi wake huyo kufana katika mashindano hayo ya kanda.

Mwanafunzi mwingine wa chuo hicho, Hudheifa Mohammad Ahmed, alitunukiwa zawadi ya Sh40,000 kwa kushinda kitengo cha kuhifadhi juzuu 20.

Mshindi wa pili kati – ka kitengo hicho alikuwa msichana Rahila Ali Ahmad aliyeshiriki kibinafsi na kuzawadiwa Sh35,000.

Katika kitengo cha kuhifadhi juzuu 10, washindi wote wawili walikuwa wasichana.

Mshindi wa kwanza alikuwa mshiriki wa kibinafsi Asya Mohammad, aliyepata zawadi ya Sh30,000.

Nambari mbili alikuwa Suheila Mohammad wa madrasa ya Darul Maarif aliyepata Sh25,000.

Mshiriki mwingine wa kibinafsi Salma Abdulkadir aliibuka mshindi wa kitengo cha kuhifadhi juzuu tano, ambapo alituzwa Sh20,000.

Nambari mbili katika kitengo hicho alikuwa Ab – dulaziz Ghalib wa madrasa ya Hudaa aliyetunukiwa Sh15,000.

Kauthar Ibrahim wa Darul Maarif alishinda tuzo ya Sh10,000 akiwa mshindi wa kitengo cha kuhifadhi juzuu mbili.

Hassan Anwar wa madrasa ya Fauz wa Salaam aliibuka katika nafasi ya pili na kutuzwa Sh5,000.

Mashindano hayo yamedhaminiwa na wakfu wa The Noble Foundation kupi – tia kwa mhisani wake Nabil Khamis, ambaye amejitosa kuwania kiti cha Mwakilishi wa Wadi ya Majengo/Mwembe Tayari katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9 kupitia tiketi ya United Democratic Alliance (UDA).

Khamis alisema wakati huu wa mwezi wa mfungo wa Ramadhan ameonelea adhamini mashindano hayo kwa ajili ya kuwapa vijana wa wadi hiyo fursa ya kudhihirisha ukwasi wao katika kuhifadhi Kuran tukufu.

Jumla ya Sh480,000 zilitumika kwa zawadi za mashindano hayo.

“Nimefurahia mno jinsi mashindano yaliendeshwa na InshaAllah The No – ble Foundation itadhamini mashindano kila mwaka,” akaeleza Khamis aliye mwana wa aliyekuwa diwani wa Majengo, marehemu Khamis Salim.

Ustadh Mohammad Ali, ambaye ni mwalimu mkuu wa madrasa ya Islahi Islamiya, asema madrasa yake pamoja na yale ya Dar Naim ndizo zilitayarisha mashindano hayo.

Ustadh Ali pia alitoa shukrani zake kwa wadhamini wa mashindano hayo The Noble Foundation, akise – ma wanafunzi, wazazi na waumini wengine wa dini ya Kiislamu waliohudhuria walikuwa na wakati mzuri.

Mwaniaji kiti cha ugavana Mombasa kwa tiketi ya UDA, Hassan Omar, pia alihudhuria na kuchangia hela zilizotumika mashindanoni.