Connect with us

General News

Mashirika yapinga mswada wa Huduma Namba – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mashirika yapinga mswada wa Huduma Namba – Taifa Leo

Mashirika yapinga mswada wa Huduma Namba

Na JURGEN NAMBEKA

MASHIRIKA 17 likiwemo lile la Kutetea Haki za Binadamu (KHRC) yanalitaka Bunge lisimamishe mjadala wa Mswada wa Huduma 2021, yakidai hauwajali Wakenya.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Afisa Mkuu Mtendaji wa Jukwaa la Haki la Wanubi Bw Shaffie Ali Hussein, alionya kuwa kupitisha mswada huu kutawanyima nafasi Wakenya wasio na vyeti vya usajili kupata huduma za serikali.

“Mimi ninawawakilisha Wanubi, Wamakonde na Wapemba ambao mswada huu utawaumiza. Afisini mwangu nina kadi ya kusubiri Kitambulisho ambacho kimechukua miaka kumi. Mswada huu haujaeleza ni vipi watu wanaopata shida za kujisali kuwa Wakenya watapata Huduma Namba,” alieleza Hussein.

Mswada wanaoupinga unanuia kuhakikisha kuwa data ya kila Mkenya imewekwa katika Mfumo wa Kitaifa wa Kusimamia Vitambulisho Jumuishi (NIIMS).

NIIMS itahakikisha kuwa data za msingi kama alikozaliwa Mkenya na data ya utendaji inayohusu usajili wa pasi za usafiri na leseni za kuendesha gari, na nambari ya kulipia kodi zipo kwenye kadi moja.

Mswada huo unalenga kuwapa Wakenya Huduma Namba ambayo itawaruhusu kupata huduma kwenye afisi za serikali.

Kulingana na KHRC, mswada wa Huduma 2021 hauangazii shida kuu ya mageuzi ya mfumo wa utambulisho na una tashwishi.

Afisa Mipango wa KHRC Bw Robert Waweru, alilamika kuwa kuwalazimisha Wakenya wote kuchukua Huduma namba bila ya kuhakikisha kuwa mfumo wa kupata vyeti vya usajili haujashughulikiwa, ni njia moja ya kuwatenga Wakenya kadhaa.

“Iwapo mswada huu hautasimamishwa kama tunavyoomba, Wakenya ambao wanasumbuka kupata vyeti vya usajili hadi wa sasa watanyimwa haki. Ni vyema mswada uondolewe Bungeni, na kamati iundwe kuhakikisha maslahi ya Wakenya wote yanashughulikiwa.

Bw Hussein aliongeza kuwa kuondoa taasisi zinazoshughulikia usajili sasa hivi, kama vile idara ya usajili wa vizazi na vifo, Kitambulisho cha Taifa, Daftari Jumuishi la Idadi ya Watu (IPRS) na Uhamiaji na kuweka majukumu hayo kwa katibu mkuu kutaathiri vikubwa usajili wa watu nchini.

Huku ikisalia miezi sita kabla ya uchaguzi mkuu washikadau hao walisema kuwa uwezekano wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka kutumia huduma namba kuwasajili Wakenya kunaweza kuathiri shughuli nzima ya uchaguzi kwa kuleta mkanganyiko.

Bw Hussein alieleza kuwa kuna njama ya kutumia mswada huo kuwanufaisha watu kadhaaserikalini akidai kuwa hata kesi waliyowasilisha kortini bado haijulikani itasikizwa lini.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending