Connect with us

General News

Mawaziri wakwepa kikao cha Dkt Ruto kujadili masuala ya usimamizi wa fedha katika serikali za kaunti – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mawaziri wakwepa kikao cha Dkt Ruto kujadili masuala ya usimamizi wa fedha katika serikali za kaunti – Taifa Leo

Mawaziri wakwepa kikao cha Dkt Ruto kujadili masuala ya usimamizi wa fedha katika serikali za kaunti

NA CHARLES WASONGA

MAWAZIRI wanaoegemea mrengo wa muungao wa Azimio La Umoja-One Kenya Jumanne, Mei 31, 2022 walikwepa mkutano wa Baraza la Bajeti na Uchumi (IBEC) ulioongozwa na Naibu Rais Dkt William Ruto katika makazi yake rasmi, Karen, Nairobi.

Mkutano huo wa 17 wa baraza hilo, uliandaliwa kujadili mikakati itakayowezesha serikali za kaunti kuimarisha ukusanyaji wa mapato.

Kiwango cha ukusanyaji mapato hayo kimekuwa kikipungua katika miaka ya hivi karibuni hali inayofanya serikali 47 za kaunti kutegemea mgao wa fedha kutoka Serikali Kuu.

Dkt Ruto alikuwa amewaalika mawaziri Ukur Yatani (Fedha) ambaye huwa ni naibu mwenyekiti wa IBEC, Eugene Wamalwa (Ugatuzi) na Peter Munya (Kilimo) lakini hawakufika.

Hata hivyo, Bw Yatani amesafiri nje ya nchi kwa shughuli za kikazi na alituma maafisa wa wizara yake kumwakilisha katika mkutano huo.

Wengine ambao hawakuhudhuria mkutano huo ni Mwenyekiti wa Tume ya Ugavi wa Mapato (CRA) Jane Karingai, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Nancy Gathungu na Msajili wa Idara ya Mahakama Anne Amadi.

Mwenyekiti wa Baraza la Magavana (CoG) na Gavana wa Embu Martin Wambora pia alikosa kuhudhuria mkutano huo wa baraza la IBEC.

Bw Wambora, ambaye anahudumu muhula wake wa pili na wa mwisho, anaegemea mrengo wa Kenya Kwanza.

Kwa upande mwingine,  mawaziri Yatani, Munya na Wamalwa wanaegemea mrengo wa Azimio la Umoja One Kenya.

Ni gavana wa Turkana Josphat Nanok ndiye gavana wa pekee aliyehudhuria mkutano huo ambao ni wa mwisho kabla Wakenya kuelekea debeni kuwachagua viongozi wapya Agosti 9, 2022.