[ad_1]
Mboko atumai uaminifu kwa ODM utampa kiti
NA WINNIE ATIENO
MBUNGE wa Likoni, Bi Mishi Mboko, ameeleza matumaini ya kupata tikiti ya ODM kuwania tena ubunge kwa msingi wa uaminifu wake kwa chama hicho.
Kulingana naye, uaminifu kwa kinara wa ODM Raila Odinga, na Gavana wa Mombasa, Bw Hassan Joho ulichangia pakubwa kwake kuinuka kisiasa.
“Mahasimu wangu wanaogombea kiti cha ubunge tupatane kiwanjani Likoni ambako tutakanyagana. Sisi tumekaa kwenye ulingo wa siasa kwa muda sana na hatubabaishwi,” alisema Bi Mboko.
[ad_2]
Source link