Mbunge John Waluke na mshtakiwa mwenzake Grace Wakhungu wakati wa kuskizwa kwa kesi yao. Picha: Standard Source: Original
Kundi hilo, miongoni mwao aliyekuwa seneta wa Kakamega Boni Khalwale, lilinyenyekea miguuni mwa Bwana kuomba mkono wake katika kesi ya Waluke.
Waluke anatarajiwa kurudisha kesi mahakamani baada ya korti ya masuala ya ufisadi kumpata na hatia na kumfunga miaka 67 au alipe faini ya zaidi ya bilioni moja.
Khalwale Jumapili ndiye alikuwa wa kwanza kutangaza kuwa walikuwa wakutane kwa maombi kumuuliza Mungu amuondolee mbunge huyo masaibu.
Mawakili wa Waluke watakuwa mahakamani Jumanne, Julai 21 kukata rufaa wakisema kulikuwa na dosari kwenye hukumu iliyotolewa.
Mawakili hao wamekuwa wakipuuzilia mbali uamuzi wa mahakama na kusema ushahidi wa upande wa mashtaka haukuwa na uzito wa kufanya jaji aafikie uamuzi aliotoa.