[ad_1]
Kura: Mchujo katika ODM utakuwa huru – Mbadi
NA GEORGE ODIWUOR
CHAMA cha ODM sasa kitatumia mchujo utakaokuwa na uwazi kupata mgombeaji maarufu wakati wa uteuzi hasa katika maeneo ambayo kuna ushindani mkali kati ya wawaniaji.
Hii ni baada ya kutangaza kuwa wanachama wake watapewa nafasi ya kumteua mgombeaji wanayemtaka kupeperusha bendera ya chama ili kupata nafasi ya kuwawakilisha raia kwenye uchaguzi wa Agosti 9.
Kumekuwa na maswali kuhusu mbinu ya uteuzi ambayo ODM inapanga kutumia kwenye mchujo.
Mwenyekiti wa ODM John Mbadi alisema ODM sasa itakumbatia mchujo na katika maeneo mengine, maafisa wa mashinani wa chama watakutana na kuamua nani anafaa kupokezwa tiketi ya moja kwa moja.
Mbinu nyingine ambayo ODM inapanga kutumia ni kuwapa tiketi wawaniaji ambao wameorodheshwa kifua mbele na tafiti zinazoendeshwa na kampuni mbalimbali japo hili limekuwa likipingwa na baadhi ya wanasiasa.
Hata hivyo, Mbunge Mwakilishi wa Kike Gladys Wanga ambaye analenga kiti cha ugavana Homa Bay, alisema ataridhia mbinu yoyote ile ambayo itatumika na chama huku akishikilia ndiye mgombeaji ambaye anafaa zaidi kutokana na rekodi yake ya maendeleo.
“Chama kinafaa kutuhakikishia uteuzi utakuwa huru. Inasikitisha kuwa baadhi ya viongozi sasa wanajigamba kuwa watafanya kila wawezalo kupata tiketi ya chama hata kama ni kuiba cheti hicho,” akasema Bi Wanga.
Akizungumza mjini Sindo alikoandaa mkutano wa kujivumisha, Bw Mbadi alisema ODM itatoa masanduku na karatasi za kupiga kura kwa wanachama wake wakati wa mchujo.
Next article
TUSIJE TUKASAHAU: Waziri James Macharia asije akasahau kuwa…
[ad_2]
Source link