Mkulima wa eneo la Kianie, Machakos anakadiria hasara baada ya mfanyakazi wake kuingia shambani ka kung’oa mboga zote alipokosa kumlipa mshahara wa miezi mitatu.
Duru zinaarifu kwamba baada ya lofa kumsababishia mwajiri wake hasara hiyo alitoweka.
Mboga shambani. Picha: TUKO.co.ke. Source: Original
Kwa mujibu wa Taifa Leo, mfanyakazi huyo anasemekana alitambulika na wengi kwa bidii yake kazini lakini mwajiri wake alikuwa akimpuuza kila mara alipoitisha mshahara wake.
Hata hivyo, jamaa alipochoka hudai hela zake alizua kioja alipofika kwa mdosi wake akafululizi hadi shambani na kung’oa mboga zote alizopanda kabla ya kuchukua virago na kuondoka.