-Olunga alifungua ukurasa wa mabao kunako dakika ya 19 na kisha baadaye kuongeza bao lingine na kuweka Kashiwa kifua mbele
– Ushindi huu ni wa kwanza kwa Kashiwa tangu kuanza kwa msimu mpya baada ya kupoteza mechi nne
-Kashiwa wamepanda hadi kwenye nafasi ya 14 na pointi tatu kutoka kwa mechi tano walizocheza
Mkenya Michael Olunga alifungia Kashiwa Resyol mabao mawili na kuwasaidia kuichapa Shonan Belmare 3-2, katika mechi ya Ligi ya Japan iliyosakatwa katika uchanjio wa Sankyo Frontier Kashiwa Jumamoi, Julai 19 mchana.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Gor Mahia alifungua ukurasa wa mabao kunako dakika ya 19 na kisha baadaye kuongeza bao lingine na kuweka Kashiwa kifua mbele kwa 2-0 kabla ya muda wa mapumziko.
Temma Matsuda ndiye alifungia Belmare bao la kwanza dakia ya 63 huku Hayato Nakama akipiga msumari wa mwisho kwenye jeneza la Reysol na kufanya matokeo kuwa 3-1 dakika saba baadaye.
Naoki Ishihara alisawazishia Belmare bao lingine dakika sita kabla ya kutaatika kwa mechi hiyo lakini halikuosha kuzamisha Reysol.
Ushindi huu ni wa kwanza kwa Kashiwa tangu kuanza kwa msimu mpya baada ya kupoteza mechi nne na sasa wamepanda hadi kwenye nafasi ya 14 na pointi tatu kutoka kwa mechi tano walizocheza.
Kashiwa sasa itavaana na Urawa Reds katika uwanja wa Saitama siku ya Jumatano mchana.
Olunga alifungia klabu hicho mabao 27 msimu uliopita na kuwasaidia kupandishwa ngazi hadi kuingia kwenye ligi J1.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.