Connect with us

General News

Mikakati ya serikali kukabiliana na baa la njaa haijazaa matunda yoyote – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mikakati ya serikali kukabiliana na baa la njaa haijazaa matunda yoyote – Taifa Leo

TUSIJE TUKASAHAU: Mikakati ya serikali kukabiliana na baa la njaa haijazaa matunda yoyote

MNAMO Alhamisi wiki hii, serikali kupitia afisi ya msemaji wake, Cyrus Oguna, ilisema jumla ya Wakenya 2.8 milioni wanakabiliwa na baa la njaa katika kaunti 23 nchini.

Hii ni licha ya kwamba ripoti ya shirika la Oxfam International kuhusu njaa nchini iliyotolewa wiki jana inasema idadi ya wanaoathiriwa na njaa imefikia 3.1 milioni.

Lakini tusisahau kuwa mnamo Februari 22, 2022 Rais Uhuru Kenyatta alizindua shehena ya chakula cha msaada cha kusambazwa kwa waathiriwa wa njaa katika kaunti zilizoathirika.

Japo, kiongozi wa taifa aliongeza kuwa serikali itatekeleza mikakati ya kudumu ya kudhibiti makali ya ukame na njaa katika maeneo hayo kame nchini, hali haijaimarika.

Ongezeko la idadi ya waathiriwa wa njaa kutoka 2.1 milioni mwaka jana hadi zaidi ya 2.8 milioni linaashiria kuwa mikakati hiyo haijazaa matunda yoyote.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending