Connect with us

General News

Mila, itikadi zinazokandamiza akina mama Pwani zipuuzwe – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mila, itikadi zinazokandamiza akina mama Pwani zipuuzwe – Taifa Leo

VALENTINE OBARA: Mila, itikadi zinazokandamiza akina mama Pwani zipuuzwe

NA VALENTINE OBARA

WAANDISHI, watunzi wa mashairi, waimbaji, waigizaji na hata wasomi kote ulimwenguni kwa miaka mingi wamekuwa wakizungumzia nguvu na uwezo wa mwanamke kuleta ufanisi katika jamii.

Mwanamke amethibitishwa kuwa kiumbe mkakamavu katika kuogelea kwenye mawimbi makali katika ulimwengu huu wenye changamoto tele.

Kwa kutaja tu wimbo wa ‘Strength of a Woman’ ulioimbwa na msanii maarufu wa kimataifa, Shaggy, ambao ni wa kuvutia kwa namna anavyomiminia sifa wanawake, wakati mwingine huwa inastaajabisha ikiwa Maulana ni wa jinsia ya kike kwa vile wamefanana kwa mema kama vile upendo na uvumilivu.

Hakika, kuna sababu ya wengi kuwafananisha viumbe hao na malaika.

Licha ya haya yote, mwanamke bado amesalia kuwa katika kikundi cha watu waliotengwa kimaendeleo na hupitia dhuluma chungu nzima, sio tu nchini pekee bali kote ulimwenguni.

Ukanda wa Pwani ya Kenya ni kati ya maeneo ya nchi ambapo mila na desturi za jadi bado ni kizuizi kwa mafanikio ya wanawake.

Ingawa kuna mikakati ambayo imekuwa ikiendelezwa kuinua hali ya maisha ya wanawake, juhudi zaidi zinahitajika kuwakweza wanawake hadi wafikie kiwango cha ufanisi kinachostahili.

Sikatai kuna mengi ambayo yamefanikishwa kufikia sasa. Tofauti na zamani, tumeshuhudia idadi ya wanawake wa asili ya Pwani ikiongezeka katika nafasi kubwa za uongozi serikalini, usimamizi wa mashirika muhimu ya kiserikali na biashara, ustadi wa kitaaluma miongoni mwa sekta nyingine. Mojawapo ya nyanja muhimu ambazo bado hatujaona wanawake wa Pwani wakichangamkia ipasavyo ni katika siasa.

Sawa na kaunti nyingine nchini ambapo itikadi za kale kuhusu uongozi zimekita mizizi, jamii nyingi za kaunti sita za Pwani bado hushikilia imani kuwa nafasi kubwa za uongozi zinastahili kuendea wanaume. Hali hii imevurugwa zaidi na kuwepo kwa wadhifa wa mbunge mwakilishi wa kaunti, kwa kuwa wanasiasa kadha wa kiume wanatumia nafasi hiyo kueneza propaganda kuwa sasa mwanamke hafai kupewa nafasi nyingine ya kuongoza kaunti kama vile ugavana au useneta.

Mwaka huu, tofauti na vipindi viwili vilivyopita vya ugatuzi, kinyang’anyiro cha ugavana katika kaunti za Pwani kimevutia idadi kubwa mno ya wanawake.

Kinachosikitisha ni kuwa, wengi wao bado wanalazimika kutegemea umashuhuri wa viongozi wengine wa kiume wanapoendeleza kampeni zao. Bila shaka, hatua hii ina uwezo wa kuwafanya wawe mateka au vivuli vya viongozi hao wa kiume, endapo watafanikiwa kushinda uchaguzini.