Wazee wa kijiji katika eneo la Mirera, Naivasha waliachwa wakijikuna vichwa baada ya kipusa kuwaeleza kuwa mumewe amekuwa akimhepa kitandani kwa miaka tisa.
Inasemekana wakwe wa kipusa waliapa kumrejesha kwa wazazi wake kwa kukosa kumzalia kijana wao mtoto lakini waliachwa vinywa wazi walipogundua ni mwanao alikuwa akimkausha mke asali kwa miaka tisa.
Picha ya wapenzi wakiwa wamenuna kitandani. Picha: Getty Images. Source: UGC
Kulingana na Taifa Leo, demu alikuwa amejaliwa mtoto kabla ya kufunga ndoa na jamaa lakini alishangaza alipokosa kuonyesha matunda ya ndoa kwa miaka tisa na ndiposa wakwe zake wakaanza kumlaumu.
Hata hivyo, kipusa aliamua kuwafungukia wazee waliokuwa wamemuandalia kikao wakitaka kujua sababu yake kuwanyima wakwe zake wajukuu.
Dada aliwaambia wazee jinsi jamaa alivyokuwa akilala kwenye sofa kila usiku na kumwacha kitandani pekee yake akisema hataki kusmbuliwa.
“Nimezoea kuishi kama binti asiyejuwa na mume kwa sababu kijana wenu alikataa katakata kunipa haki ya ndoa. Yeye hudai cha muhimu ni kunipa mali na kulea binti yangu. Nimekuwa nikivumilia tu kwa sababu sikutaka kumuaibisha,” mama alifunguka.
Inasemekana maneno ya mama yaliwaacha wazee midomo wazi huku juhudi zao za kumtaka lofa kujieleza kuhusiana na madai hayo zikigonga mwamba.
“Kama mke hajalalamika sioni haja ya mtu kuingilia maisha yetu. Wanaodai wanataka wajukuu watosheke na huyu binti mmoja ambaye tumejaaliwa. Hayo mengine mtuachie tutasuluhisha,” jamaa aliwaambia wazee.