– Hamisi Taletale, almaarufu kama Babu Tale, amempoteza mke wake
– Shamsa Tale alithibitishwa kuaga dunia siku ya Jumapili, Juni 28, kama alivyoeleza mama yake Diamond
– Mama Dangote alipakia ujumbe wa rambi rambi kwa familia huku akiwaombea wapate nguvu kutoka kwa Mwenyezi Mungu
Meneja wa lebo ya Diamond Platnumz ya Wasafi Classic, Baby Hamisi Taletale, almaarufu kama Babu Tale, amempoteza mke wake.
Habari hiyo ilifichuliwa na mama yake Diamond, Mama Dangote, ambaye alisema alikata roho asubuhi mapema Jumapili, Juni 28 asubuhi.
Mama Dangote pia alipakia picha ya Shamsa Tale akiwa pamoja na mume wake huku akiomboleza kifo chake.
“Mke na mama watoto wa meneja wa lebo ya WCB Hamis Taletale, Shammy alifariki mapema hii leo,” aliandika mama huyo.
Aliomboleza na familia hiyo huku akiwaombea nguvu wakati huu mgumu.
“Tunatuma salamu zetu za rambi rambi kwa familia ya ndugu wetu Hamis Taletale wakati huu mgumu na tunamuombea Mungu amupe nguvu na uponyaji,” aliongezea Mama Dangote.
Kufikia sasa bado chanzo cha kifo chake hakijafichuliwa na familia yake pia bado haijazungumzia rasmi suala hilo.
Kenyan Digest inatuma salamu zake za rambi rambi kwa familia na marafiki wa Hamisa Taletale.