– Mlinzi huyo alikuwa aandamane na gavana Joho kwenda Dubai kumtembelea Raila Odinga hospitalini ila alizuiwa baada ya kupatikana na virusi vya COVID-19
– Walinzi wengine wanne wa Joho wamewekwa karantini ya lazima baada ya mmoja wao kupatikana na virusi hivyo
– Hata hivyo, haijabainika iwapo gavana Joho pia amekutwa na virusi hivyo kwani alitangamana na walinzi hao
– Imeripotiwa kuwa Joho hufanyiwa vipimo vya COVID-19 kila baada ya wiki moja
Mmoja wa walinzi wa Gavana wa Mombasa Hassan Joho ameripotiwa kupatikana na virusi vya COVID-19.
Kwa mujibu wa taarifa za K24, mlinzi huyo anasemekana kukutwa na virusi hivyo akiwa jijini Nairobi ambapo alikuwa ameagizwa kumsubiri gavana Joho ili waandamane naye kumtembelea Raila Odinga nchini Dubai.