– Mkutano wa Peter Kenneth na kundi lake ulimkera Seneta Kang’ata akisema ulikuwa ukipanga kutwaa uongozi wa Rais Uhuru katika jamii ya Mlima Kenya
– Amekashifu kundi hilo na kulinganisha hatua yao na watoto wakorofi wanaotaka kumrithi baba akiwa hai
– Hata hivyo kundi hilo lilisema kikao chao kilikuwa cha kutoa shukrani kwa Rais kwa kuwapa wadhifa wa kiongozi wa wengi
Kiranja wa wengi katika Seneti Irung’u Kang’ata amekashifu viongopzi ambao walifanya mkutano katika mkahawa wa Panafric Jumatano, Juni 8 kujadili siasa za Mt Kenya.
Mkutano huo uliongozwa na Peter Kenneth na kujumuisha magavana kadhaa kutoka Mlima Kenya, maseneta, Spika wa Bunge Justin Muturi na kiongozi wa wengi Amos Kimunya.
Kiranja wa wengi Irung’u Kang’ata. Kang’ata alisema hakuna mtu atafaulu kumtwaa Rais Uhuru Kenyatta kama kigogo wa Mt Kenya. Picha: Citizen Source: UGC
Kang’ata alisema Rais Uhuru Kenyatta atasalia kuwa kigogo wa Mt Kenya na ni makosa kwa yeyote kuketi kupanga njama ya kuchukua usukani wa Mlima Kenya kisiasa.
Akizungumzia mkutano huo wa Panafric, Kang’ata alitumia mafumbo ya jamii ya Kikuyu kupuuza kundi hilo la Panafric.
“Hakuna mkutano katika mkahawa au ukumbi wowote ambao utapanga njama ya kuchukua nafasi ya kigogo wetu wa Mt Kenya,” alisema Kang’ata.