Connect with us

General News

Mondi afukuzia kolabo na RiRi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mondi afukuzia kolabo na RiRi – Taifa Leo

KASHESHE: Mondi afukuzia kolabo na RiRi

NA SINDA MATIKO

DIAMOND Platnumz ameanza kufukuzia kolabo na staa wa RnB badgirl RiRi.

Kwa sasa, Platnumz kahamishia kambi yake Marekani ambapo juzi aliandaa pati ya kuwasikilizisha watu EP yake mpya First Of All aliyoachia wiki tatu zilizopita.

Akiwa bado yupo huko Marekani, Diamond kafanya mahojiano na BBC na kufichua mchakato anaoendelea nao wa kufanya kitu na Rihanna.

“Ningependa kufanya kazi na Rihanna. Nahisi itakuwa ngoma kali sana. Kama sio kwenye albamu hii basi albamu yangu inayofuata. Tumeshaongea na Rihanna na timu yake na kila kitu kipo sawa,” Diamond aliiambia BBC.

Hata hivyo, aliishia kudokeza kwamba huenda ushirikiano huo ukachelewa kutokana na hali ya Rihanna ambaye ni mjamzito.

Rihanna hajatoa albamu au wimbo wowote kwa miaka minne sasa. Kulikuwepo na ripoti kwamba alipania kuachia albamu mwaka huu baada ya kujifungua.

Katika kupanua mawanda yake, Diamond ameendelea kufukuzia kolabo na mastaa wa kimataifa akiwa tayari ameshafanya kazi na Neyo, Rick Ross na Omarion.